Na Mwandishi Wetu
Watanzania wametakiwa kuangalia ubora elimu
katika vyuo vya nje na sio kuangalia majina ya vyuo hivyo ili ukuweza kupata
wataalamu wataosaidia nchi kupata maendeleo.
Hayo aliyasema jana,Mkurugenzi Mtendaji wa Global
Education Link,Abdulmaliki Mollel katika maonesho ya Elimu ya Vyuo Vikuu vya Ndani na Nnje ya nchi
yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mollel amesema yeye akiwa wakala wa vyuo vikuu
vya nje anatambua vyuo walivyoenda watanzania kusoma hawakumuangusha kutokana
na kujituma kwao pamoja na mazingira rafiki ya kusomea katika vyuo hivyo.
Amesema watu wanaokwenda katika vyuo kwa
kuangalia majina wanarudi na kuwa hawana msaada wa elimu walioipata nje na
kulazimika nchi kuchukua wataalam kutoka nje wenye uwezo kutokana na vyuo vyao
na kuacha watanzania waliopata elimu katika vyuo vyenye majina lakini havina
elimu bora.
Mollel amesema kuna vyuo vingi nje lakini suala
la kuangalia ubora wa elimu inayotolewa na mazingira ya kusomea kutokana na
baadhi ya watu waliosoma wamekuwa wakiiga utamaduni mwingine na kuingiza nchini
na kushindwa kuendana na utamaduni wa ndani na kusababisha kukosa ajira.
Mollel amewataka watanzania kutumia Global
Education Link katika kuweza kuwapa vyuo bora ambavyo itasaidia vijana kupata
elimu bora kutokana na uwezo wa vyuo husika.
Aidha amesema Global Education Link imekwenda
mbali zaidi kwa baadhi ya vyuo vya nje kuingiza kozi katika vyuo vya ndani
ikiwemo kozi ya Petrol ,Gesi.
Amesema
anafanya kazi na vyuo 10 vya nje ambavyo vinazalisha elimu bora yenye
kumsaidia mtanzania katika kuweza kuongeza uwezo wa kitaalam katika nchi.
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa shirika la taifa la bima (NIC), Sam Kamanga akipata maelezo kutoka kwa afisa masoko mwandamizi wa shirika la taifa la bima (NIC),Joyce Mswia katika maoneho ya wiki ya elimu ya vyuo vikuu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Da es Salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa Global Education Link akiwapa maelezo wananchi alipotembelea banda la Global Education Link katika maoneho ya wiki ya elimu ya vyuo vikuu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Da es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...