Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hundi ya malipo ya Bima ya Maisha(Flexi Provider) kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa(National Insurance Corporation of Tanzania Limited) NIC Bwana Sam Kamanga Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Akimkabidhi hundi hiyo,  Bw. Sam Kamanga amesema uwepo wa Mheshimiwa Rais kama mteja wa NIC imesaidia kukuza uelewa na shughuli za shirika hilo.
“Kitendo cha Serikali kukatia Bima mali zake na taasisi zake, kumeongeza uwezo wa kifedha wa shirika na soko la Bima” amesema na kuwataka watu binafsi, taasisi mbalimbali na mashirika ya kiserikali kukata Bima kwa ajili ya maendeleo na akiba ya baadaye. 
Rais Kikwete ameitaka NIC kuongeza juhudi katika kuhamasisha na kuelimisha watanzania umuhimu na manufaa makubwa yanayopatikana kutokana na Bima.
Picha na Freddy Maro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2015

    How does zat work? I thought ni mpaka ufe ndiyo life insurance inakuwa paid out?

    Hi guys what life insurance is zat in Bongoland?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2015

    sio lazima ufe kuna watu wengine huwa hawafi kiurahisi kwa hiyo ipo aina ya bima ambayo unaweza kukopa fedha baada ya kuwa na bima hiyo kwa miaka Fulani au kuchukua fedha kiasi Fulani moja kwa moja kinacho tokana na asilimia ya fedha uliyotumia kukatia bima yenyewe kwa miaka kadhaa mara nyingi huwa miaka 20 au zaidi,sasa sielewe hii ya mheshimiwa ni ipi kati ya hizi mbili kwa sababu kama unavyoona bado yu hai na mzima wa afya mungu ampe umri mrefu zaidi bado tuna muhitaji.

    mdau.

    misungwi,mwanza.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2015

    National Insurance Corporation (T) ina products nyingi za Bima. Mheshimiwa alichukua Bima ya maisha ambayo inaitwa (Flexi Provider). Bima hii iko tofauti sana na Bima nyingine za Life Insurance ambazo wadau wngi wa ughaibuni mnazozifahamu (Kila soko lina product zake). Kwa maswali zaidi juu bidhaa zetu mbali mbali za Bima naomba ututumie email kwenye address hii
    info-nic@nictanzania.co.tz ni matumaini yetu utakipenda chako kwa kuchukua Bima katika shirika la Bima la Taifa (Tanzania).

    Big up for Mr. President kwa kuonyesha uzalendo wa hali ya juu na kulipa support shirika la umma.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...