Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete kwa kushirikiana Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Kidemkrasia ya Ethiopia leo Bw. Hailemariam Desalegn (Alhamis) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kiwanda cha Viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu wanaoeneza malaria kilichopo Mjini Kibaha,mkoani Pwani.
Kiwanda hicho kimejengwa na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwa kushirikiana na kampuni ya LABIOFAM ya Cuba.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa NDC Bw Mlingi Mkucha imesema Waziri Mkuu Bw Desalegn ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Viongozi wa Kiafrica Dhidi ya Ugonjwa wa Malaria(ALMA).
Aidha wageni wengine kwenye hafla hiyo ni Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mwenyekiti wa Bodi ya Roll Back Malaria Partnership Dkt. Victor Makwenge Kaput, pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Cuba nchini Tanzania.
Aidha, uzinduzi huo pia utahudhuriwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdala Kigoda Katibu Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue, Makatibu Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Bw Mkucha amesema katika taarifa hiyo kuwa, kiwanda hicho ambacho ni cha kwanza na cha aina yake hapa nchini na Afrika kwa ujuml, kimejengwa kufuatia ziara ya Rais Kikwete nchini Cuba mwaka 2009, ambapo aliiagiza NDC ijenge kiwanda cha namna hiyo nchini kwa kutumia uzoefu wa huko Cuba.
“Ujenzi wa kiwanda hicho unalenga kutimiza ahadi ya Rais Kikwete ya kutokomeza ugonjwa hatari wa malaria nchini, kwa kuwa kinategemewa kutoa ufumbuzi wa kudumu kwa ugonjwa wa malaria,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
“Viuadudu vitakavyozalishwa kiwandani hapo vinalenga kuua viluwiluwi vya mbu hao katika mazalia yake hivyo kukatisha maisha ya mbu akiwa katika hatua ya kiluwiluwi na matokeo yake ni kutokomeza malaria nchini” imefafanua.
Kwa upande mwingine, kiwanda kitakuwa na ushirikiano na Taasisi za Utafiti na Vyuo Vikuu nchini, ili kuzipatia fursa za kutumia maabara za kisasa zilizoko kiwandani, hivyo kuongeza ujuzi wa kufanya tafiti mbalimbali na kubuni na kuzalisha bidhaa zingine za kibaiolojia.

ReplyDeleteNajua ku-blog sio sehemu ya journalism ni usanii wa kuandika, mfano wa barua.
Lakini wekeni picha zinazowiana na wakati wa uzinduzi; sio hiyo ya Ulaya!