Tungependa kuwatangazia wanajumuiya wetu, Watanzania wanaoishi Manchester na Watanzania wanoiishi miji ya karibu kama Liverpool, Leeds, York na Newcastle kwamba utakuja Kamati kutoka Ubalozi wa Tanzania kwa hapa Uingereza kwa ajili ya zoezi la ku renew pasipoti.

Hili zoezi litafanyika Jumamosi hii inayokuja, tarehe 11 / 07 / 2015 kuanzia saa sita mchana mpaka saa tatu za usiku ( 12:00pm - 9:00pm / 12:00hrs - 21:00hrs). 

Hili zoezi litafanyika anuani ifwatayo:
Trinity House Community,
Resource Centre,
Grove Close,
Rusholme,
Manchester,
M14 5AA.

Tafadhali wasiliana nasi kwa 
maelezo zaidi au bonyeza link ifwatayo:


Tafadhali mjulishe na mtanzania mwenzako.
Asanteni Sana.
Bravo Mkony
Mwenyekiti
TAGMA
Kwa maelezo zaidi tafadhali piga simu zifwatazo:
Bravo Mkony ( Mwenyekiti, TAGMA) - 07740 980525
Tilumanywa Mkama ( Makamu Mwenyekiti, TAGMA) - 07747 181630
Lilian Mkocha ( Katibu Mkuu, TAGMA) - 07880 994315
Ally Mtiga ( Naibu Katibu, TAGMA) - 07553 282798

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 10, 2015

    Kwani nini tukisha fanya hili zowezi vitu vikifika Tanzania tuna daiwa vyeti vyakuzaliwa vya Baba na mama, ukipeleka hivyo unaambiwa ulete vya bibi au babu.

    Sasa kama nihivyo kwani nn ubalozi Uhakiki hapa halafu kule una hangaishwa.

    Mimi binafsi nili hangaishwa sana ningeli omba taasisi husika iliweke wazi jambo hili ili hawa wenzangu wasije wakapewa tabu kama niliyo pewa mimi, ikumbukwe kuwa ukiwa ugenini passport ni muhimu Sanaa.

    Natabu hizi zinakuja za nini kule Tanzania ikiwa huku ishatazamwa na sisi tuna badili tuu hizi passport.

    Asante kwa kunifikishia maoni yangu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...