Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti mjini Dodoma.(Picha na Adam Mzee)

…………………………………………………………………………

“Leo tarehe 7 mwezi wa saba tunaanza vikao vya mchakato wa mkutano mkuu wa taifa wa CCM ambao unnategemewa pamoja na mambo mengine utapitisha ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-20 20 lakini pia utateua mgombea wa urais wa jamhuri ya muungano wa tanzania kupitia CCM, na pia kutakuwa na kikao cha halmashauri kuu ambacho kitateua jina la mgombea wa urais kwa chama cha mapinduzi kwa upande wa Zanzibar, ratiba ya vikao
Leo tarehe 7 kuanzia  saa tano tutakuwa na sekretarieti ya halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi ambacho kitaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.
 "Sekretarieti hiyo ina ajenda moja kubwa kwa kupitia maandalizi ya mkutano mkuu, ina ajenda kubwa ya kupitia maandalizi ya mkutano mkuu na kuthibitisha yapo mambo mengi katika maandalizi kuna mambo ya ratiba, mambo ya malazi ya wajumbe, kuna mambo ya makablasha mbalimbali na maandalizi ya document mbalimbali zitakazotumika kwenye vikao vitakavyoendelea baada ya leo. 
"Kesho tarehe 8 kunategemewa kufanyika kikao cha kamati ya usalama na maadili cha chama, ambacho kitakuwa chini ya mwenyekiti wa Taifa  Dk.Jakaya Mrisho Kikwete. 
"Tarehe 9 kichama kutakuwa na shughuli kuu mbili. Ya kwanza asubuhi, kutafanyika uzinduzi au ufunguzi wa ukumbi mpya wa chama cha mapinduzi na ofisi zake ambao upo njia ya kwenda chuo kikuu cha Dodoma.
"Bila shaka baadhi yenu mtakuwa mmeona, mwenyekiti wa chama Rais Kikwete alipokwenda kutembelea kwa hiyo ufunguzi wake utafanyika tarehe 9, majira ya asubuhi kabla mheshimiwa Rais hajaenda kuvunja bunge.
"Kama ratiba itabadilika tutawaambia lakini tarehe 9 tuna hiyo shughuli ya kwanza baadaye mchana kutakuwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi ambayo nayo ni muendelezo wa vikao vya awali kuelekea mkutano mkuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...