Bendi mpya ya muziki wa dansi ijulikanayo kama The Stars Band iliyo chini ya Aneth Kushaba imezinduliwa rasmi siku Jumamosi ya Julai 18, siku ya Idd-Mosi ndani ya kiota cha Mzalendo Pub, Kijitonyama jijini Dar es Salaam huku ikisindikizwa na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Barnabas pamoja na bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.  
Mkurugenzi wa The Stars Band, Aneth Kushaba akijitambulisha kwa mashabiki wakenm  pamoja na azungumza na wapenzi wa bendi mpya ya The Stars Band wakati wa uzinduzi yeye binafsi alisema hawezi kusema yaliyopita bali wapenzi wa bendi hiyo wategemee makubwa kutoka kwenye bendi hiyo iliyozinduliwa siku ya Idd Mosi ndani ya kiota cha Mzalendo Pub
Mwimbaji wa Bongo Flava, Barnaba Elias aka Barnaba akiimba moja ya nyimbo zake huku akisindikizwa na waimbaji wa Bendi ya The Stars kutshoto ni Seghito na kulia ni Prince.
Waimbaji wa Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' ambao ni  Jesus(wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Patcho Mwamba(wa pili kutoka kushoto),  Pablo Masai (katikati), Mulemule(wa pili kutoka kulia) pamoja na 33 wote wakiimba kwa pamoja wakati wa uzinduzi wa bendi mpya ya The Stars katika kiota cha Mzalendo Pub 
RAIS wa bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma', Nyoshi El Sadat akiimba kwa hisia kali wakati wa uzinduzi wa bendi ya The Stars iliyofanyika kwenye kiota cha Mzalendo Pub siku ya Idd-Mosi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2015

    What is the idea of that msichana kwenda jukwaani uchi?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2015

    basata kimyaaaaaa! Ingekua nanii lazima ungewasikia!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 20, 2015

    Kina Dada lazima wajiangalia mavazi yao wanapokwenda jukwaani sio wafanye vitu nje ya maadili,na kutafuta kick ya kujadaliwa mitandaoni

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 20, 2015

    wapi basata???

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2015

    Sasa huyo dada kaenda uchi sijui ni utamaduni gani huo. Mbona mwenzake picha ya chini kavaa vizuri tena kapendeza sana. Kama ni kuuza muziki watu wananunua kwa kuangalia maadili vile vile.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...