Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa ,Allan Kijazi(wasita toka kushoto waliosimama)akiwa kwenye picha ya pamoja na Timu ya watu 39 wakiwemo Wakurugenzi wa kampuni ya Vodacom na kampuni mbalimbali za nchini Afrika Kusini kabla ya kuanza zoezi la kupanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia kununua vitambaa maalumu(Pedi) vya kuwahifadhi wasichana walioko mashuleni wakati wa hedhi.
Ofisa mkuu wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom, Afrika Kusini,Maya Makanjee(wapili toka kushoto) akiwa katika lango la kuanzia safari ya kupanda mlima Kilimanjaro,Makanjee anapanda mlima huo ikiwa ni sehemu ya changamoto ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia kununua vitambaa maalumu kwa wasichana walioko mashuleni kujisitiri wakati wakiwa kwenye Hedhi.
Ofisa mkuu wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom, Afrika Kusini, Maya Makanjee(wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mratibu wa zoezi la kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua vitambaa maalumu kwa wasichana walioko mashuleni kujisitiri wakati wakiwa kwenye Hedhi,Richard Mabaso (wa kwanza toka kushoto aliyeshika bendera),wengine ni washiriki wa zoezi hilo la kupanda Mlima Kilimanjaro kutoka mataifa mbalimbali.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...