Na Mwandishi
wetu, Dar es Salaam
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada
wa shilingi milioni mbili kwa Taasisi ya Habari Development Association kwa
ajili kuandaa mafunzo ya kuwawezesha waandishi wa habari kujenga weledi wa
kufanya tafiti na kuandika habari za kupambana na ujangili.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Awadh Massawe
alikabidhi hundi ya thamani ya fedha hizo kwa Mkurugeni wa taasisi hiyo, Bw.
Kunze Mswanyama jana jijini Dar es Salaam.
“Tunaunga mkono juhudi hizi za kupambana na ujangili,”
alisema Bw. Massawe mjini hapa.
Alisema TPA imefanya hivyo kwa kuwa nchi ina tatizo la
uwindaji haramu hasa wa ndovu na usafirishaji wa pembe za ndovu na kulisababishia
hasara taifa kupitia mipaka ya taifa.
Alifafanua kwamba bandari ya Dar es Salaam ni sehemu
ya mpaka wa taifa, hivyo lazima TPA iunge mkono juhudi za kuelimisha jamii na
kuzuia uhalifu huo.
“Tunazidi kuimarisha ulinzi katika bandari kwa kuwa ni
sehemu ambayo bidhaa haramu zinaweza kupitishwa,” alisema.
Alifafanua kuwa kwa sasa wanatarajia kufunga kamera
400 za CCTV ili kuimarisha na kuwa skana tatu zimeletwa banadarini kwa ajili
yakuziongezea nguvu skana mbili zilizopo.
Pia alisema wanatarajia kupata msaada wa mbwa maalumu
wa ulinzi watakaotolewa na serikali ya Marekani.
Alisema TPA inaendelea kuwajengea uwezo wafanyakazi
kimaadili ili kuendelea kufanya kazi kwa weledi na uaminifu kwa faida ya taifa.
Mkurugenzi wa Habari Development Association, Bw.
Mswanyama alisema fedha walizopewa watazitumia kwa kutoa mafunzo kwa waandishi
wa habari 54 wa maswala ya ujangili kupata weledi na kutafiti na kufichua
ujangili.
“Tunahitaji kujenga weledi zaidi wa kupambana na
ujangili wa rasirimali zetu ili taifa liweze kunufaika nazo,” alieleza.
Alisema taasisi yao inaundwa na waandishi wa habari
wanaoandika habari za kupambana na ujangili na rasirimali nyingine katika mbunga
mbalimbali zikiwemo za Sadani, Serengeti, Mikumi na Selou.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
nchini (TPA), Bw. Awadhi Massawe katikati akizungumza wakati alipokuwa
akikabidhi hundi ya shilingi milioni mbili(2m/-) kwa Taasisi ya Habari
Development Association, kwa ajili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kufanya tafiti na kuandika
habari za kupambana na ujangili nchini. Taasisi hiyo inaundwa na waandishi wa
habari wanaoandika habari za ujangili kwa kina. Kulia ni Mkurugenzi wa taasisi
hiyo, Bw. Kunze Mswanyama na kushoto ni Ofisa Mawasiliano Mwandamizi wa TPA,
Bw. Focus Mauki
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari nchini (TPA), Bw. Awadhi Massawe kushoto akimkabidhi hundi ya shilingi
milioni mbili (2m/-) Mkurugeni wa Taasisi ya Habari Development Association,
Bw. Kunze Mswanyama kwa ajili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa
habari kufanya tafiti na kuandika habari za kupambana na ujangili. Taasisi hiyo
inaundwa na waandishi wa habari wanaoandika habari za ujangili kwa kina.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...