Watanzania wanashauriwa kuitumia fursa hii ya kipekee ya ziara ya kitabibu itakayofanywa na madaktari kutoka Hospitali za Apollo; Hyderabad.  Kwa miaka mingi, watanzania wameshindwa kupata matibabu sahihi nchini kitendo ambacho kimewasababishia kusafiri nje ya nchi kupata matibabu sahihi ya mfumo wa fahamu, uti wa mgongo, figo pamoja na magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo. 

 Nia na madhumuni ya ziara ya madaktari na washauri hawa kutoka Hospitali za Apollo nchini Tanzania ni kuhakikisha kwamba wagonjwa wanapata vipimo sahihi kwa gharama nafuu. Madaktari bingwa watatu wanao ongoza katika Hospitali za Apollo watafanya kazi kwa kushirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Hindu Mandal kutoa huduma za kimataifa kwa watanzania.

Wagonjwa wanaougua magonjwa yanayohusiana na uti wa mgongo, mishipa ya fahamu, figo na magonjwa ya kibofu cha mkojo, wanashauriwa kuhudhuria na kushiriki tukio hili la kipekee. Madaktari watatembelea wagonjwa, kufuatilia historia za wagonjwa na kuwashauri matibabu sahihi kutokana na ripoti za matibabu na vipimo.
Daktari wa kwanza atakayeshiriki katika kutoa ushauri na matibabu ni Dkt. Alok Ranjan ambaye ni mtaalamu katika upasuaji mishipa ya fahamu na uti wa mgongo katika Hospitali za Apollo mjini Hyderabad.  Atapatikana siku ya Jumatatu ya tarehe 27 Julai na tarehe 28 Julai kati ya saa 03 asubuhi  na 11 jioni kwa tarehe hizo mbili katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...