Moja kati ya changamoto tunayokutana nayo hapa Dudumizi pindi tunapofanya kazi za wateja wetu ni kuwa, wengi wao wamekuwa wakitaka kukamilisha kazi ya kesho leo. Hii ina maana, mteja anataka website ambayo ina vitu vingi ambayo si lazima vyote vikamilike kwa siku moja.
Kwenye biashara yoyote, kama alivyoandika Simon Sinek's kwenye kitabu chake cha anza na kwanini, "Start with why" kuwa unatakiwa kuanza na sababu ya kuwepo kwa biashara yako, na si nini unatakiwa kufanya. Kwa kujua hili, kutakusaidia kujua na kupanga hatua kwa hatua cha nini kifanyike kwenye muda gani ili kukidhi mahitaji ya wateja.
Ukiangalia website nyingi maarufu duniani. kama Facebook, Twitter, Apple, Google, YouTube, eBay, LinkedIn, Yahoo, na Flickr zimekuwa zikibadilika kuendana na matakwa ya watumiaji na wakati. Hii ni kwa sababu, uwepo wao kwenye biashara unategemeana sana na mambo hayo muhimu. Kumbuka, hazina(muda na pesa) zina kikomo hivyo lazima kuwe na mpango endelevu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...