Wakazi wa Kijiji cha Kingwang’oko Tabora wapatiwa huduma za
mawasiliano na Airtel
WAKAZI wa Kijiji cha Kigwang’oko Wilaya ya Ulyankulu,wameipongeza
kampuni ya Airtel kwa kuwajengea mnara wa mawasiliano na hivyo
kuondokana na tatizo sugu la mawasiliano lililokuwa likiwakabili.
Wakazi hao wamekuwa wakifanya shughuli zao bila ya mawasiliano ya
uhakika kwa muda mrefu jambo linalotajwa kukwamisha shughuli nyingi za
maendeleo kijijini hapo.
Wanakijiji hao wameeleza kuwa, wamekuwa wakipata tabu ya kufanya
mawasiliano wakati mwingine wakilazimika kupanda kwenye miti au
vichuguu kupata mawasliano kabla ya kujengwa kwa mnara huo.
“Tunawashukuru sana Airtel kwa kutukumbuka na kutuleta mnara huu
ambao hapa kijijini kwetu ni mkombozi mkubwa katika sekta ya
mawasiliano” walisema wananchi hao
Akiongea na waandishi wa habari mkazi wa Kigwang’oko, Juma Magema
alisema
“Kabla ya Airtel kuweka mnara hapa kijiji kwetu tulikuwa
tunapanda katika miti na hata vichuguu ili kupata mawasiliano, lakini
sasa hatupati tena shida hiyo”
Akiuzindua mnara huo,aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kaliua, John Kadutu, amewataka wananchi kuutumia mnara kuboresha
shughuli zao za kijamii na kiuchumi na kuboresha maendeleo ya kijijini
hapo na jamii kwa ujumla.
“Muutumie mnara huu kujiletea maendeleo kwani hivi sasa mnaweza
kutumia mawasiliano ya Airtel na huduma zote zinazoenda sambamba na
uwepo wa mnara huo kijijini hapo” alisema Kadutu
Awali meneja wa Airtel Mkoa wa Tabora,Fidelis Lugangira,alisema
wamepeleka mnara huo ili kuboresha za kiuchumi ,lengo likiwa ni kuzidi
kuwafanya wanufaike kwa kutumia mawasiliano.
“Mnara huu umejengwa kijijini hapa ikiwa ni hatua ya Kampuni yetu
kusogeza karibu huduma za mawasiliano hivyo ni fursa ya kipekee kwenye
kujiletea maendeleo” alisema Lugakingira.
Airtel imezindua huduma ya mawasiliano katika Kijiji cha Kigwang’oko
Wilayani Ulyankulu mikoani Tabora mara baada ya kuzindua huduma kama
hizo katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida na katika kijiji cha
Nduruma wilayani Arumeru mkoani Arusha. Mpango mkakati ni kufikia
maeneo mengi zaidi husasani yaliyoko pembezoni mwa nchi
Msimamizi wa Mnara wa Airtel Tabora, Bwana Phidelis Lugangila akimwonyesha sehemu za mnara , aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, John Kadutu baada ya uzinduzi wa mnara huo wa mawasiliano wa Airtel, utakaowawezesha wakazi wa kijiji cha
Kingwang’oko wilayani Uyankulu mkoani Tabora kupata mawasiliano bora. Akishuhudia ni Diwani wa kata ya Kona nne Bwana Japhael Lufungija akifatiwa na Afisa Masoko wa Airtel Tabora, Godfrey Kigata
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa mnara huo wa mawasiliano wa Airtel, utakaowawezesha wakazi wa kijiji cha Kingwang’oko wilayani Uyankulu mkoani Tabora kupata mawasiliano bora.
Wanannchi wakifurahia baada ya uzinduzi wa mnara huo wa mawasiliano wa Airtel, utakaowawezesha wakazi wa kijiji cha Kingwang’oko wilayani Uyankulu mkoani Tabora kupata mawasiliano bora.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...