Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Kiseke Wilaya
ya Ilemela Mkoani Mwanza, wakiwa wameketi
kwenye madawati 64 yenye thamani ya shilingi milioni 5 waliyokabidhiwa na
Benki ya NMB kama sehemu ya msaada kwa shule hiyo.
Mkuu
wa Wilaya ya Busega Mkoani Mwanza Bw.
Paulo Mzindakaya , akimpa mkono wa shukurani Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB Bw.
Waziri Barnabas(kulia), baada ya kukabidhi
madawati 240 yenye thamani ya shilingi milioni .... yaliyotolewa na
benki ya NMB ukiwa ni msaada kwa Shule
za Msingi Nyashimo na Nasa Wilayani Busega pamoja na Sukuma na Simakitongo
Wilaya ya Magu ili kupunguza uhaba wa madawati katika shule hizo. Kila shule
imepata madawati sitini.
Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Kwibara wakiwa wameki kwenye madawati waliyokabidhiwa na NMB
Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Kwibara wakiwa wameki kwenye madawati waliyokabidhiwa na NMB
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mkoani Mara Bw. Zelothe Stephen , akimpa
mkono wa shukurani Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB Bw. Waziri Barnabas(kushoto),
baada ya kukabidhi madawati 330 yaliyotolewa na benki ya NMB ukiwa ni
msaada kwa Shule za Msingi Bwai, Kiriba, Chanyahuru na Busumi pamoja na
shule ya Sekondari Kiriba zilizopo Musoma vijijini ili kupunguza uhaba wa
madawati katika shule hizo. Kila shule imepata madawati hamsini na tano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...