Kaimu Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Jasper Mero akizungumza mkutano wa kupanga mikakati  ya Fedha  katika ofisi ya mdhibiti wa fedha za serikali CAG, leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa wadau wa kuandaa mikakati ya  Ofisi  ya CAG wakimsikiliza Kaimu Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Jasper Mero mkutano wa kupanga mikakati  ya Fedha  katika ofisi ya mdhibiti wa fedha za serikali CAG, leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Jasper Mero akiwa  katika picha ya pamoja na wadau wa mkutano wa wadau wa kuandaa mikakati ya  Ofisi  ya CAG leo jijini Dar es Salaam. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MALENGO ya ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inategemea na mchango wa wadau  katika kupanga mikakati ya kuwezesha  ofisi hiyo iweze kusimamia katika kuhakikisha fedha za umma zinaleta maendeleo ya kiuchumi.

Hayo ameyasema leo,Kaimu Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Jasper Mero wakati akifungua mkutano wa wadau wa kuandaa mikakati ya  Ofisi  ya CAG ya 2016 -2021 katika kuweza ofisi hiyo iweze kusimamia mikakati hiyo.

Mero amesema wananchi wanahitaji usimamizi wa fedha zao ili waweze kupata maendeleo ya kiuchumi na hiyo inatokana na ofisi ya CAG kuweka mikakati ya kuhakikisha fedha ya umma haipotei.

Amesema wadau wametakiwa kutoa maoni kwa uhuru katika ofisi hiyo iweze kupata mikakati ya kuweza kusimamia katika udhibiti wa fedha ya Umma.

Mero amesema mikakati ya 2011hadi 2016 imetekekelezwa kwa asilimia 100 hiyo ikiwa imetokana na mahusiano ya ofisi ya CAG pamoja na wadau ambao walitoa maoni chanya katika ofisi hiyo.

Aidha amesema wadau wana nafasi ya kuweka mawazo yao katika kutengeneza mikakati ya miaka mitano ambayo itafanya mabadiliko   ofisi ya CAG katika kudhibiti fedha ya umma.

Amesema katika ofisi ya CAG imepata mafanikio ikiwa ni pamoja kutoa ripoti za mara kwa mara pamoja na kutoa ushauri wa kiutekelezaji kutokana na ukaguzi walioufanya katika mashirika ya Umma ,pamoja na Taasisi za Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...