Meneja
Biashara wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Thabit
Mndeme, kushoto, akizungumza jambo wakati akitangaza taasisi yao
kuendelea kutoa huduma ya mradi wa viwanja vya Vikuruti, wilayani
Kibaha, mkoani Pwani, ulioanza Mei 22, mwaka huu na kupokewa vizuri na
Watanzania wengi. Kulia ni IT Meneja wa Taasisi hiyo, Daud Mavule.
WATANZANIA
wenye nia ya kumiliki ardhi, wataendelea kuipata fursa hiyo baada ya
Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, kuwapatia nafasi
wateja wao katika mradi huo ulioanza rasmi Mei 22 mwaka huu na
kuzinduliwa katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Hayo
yamesemwa na Meneja Biashara wa Taasisi hiyo, Thabit Mndeme, alipokuwa
akizungumza jijini Dar es Salaam, juu ya huduma hiyo ya viwanja
vinavyotolewa kwa watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na
wajasiriamali.
Kwa mujibu wa Mndeme, wameamua kuendelea kutoa huduma hiyo ya viwanja katika eneo ya Vikuruti, baada ya kufanya tathmini kwa kuangalia umuhimu wa Watanzania kuweza kumiliki viwanja ili kujenga nyumba za kuishi, nyumba za biashara na mahitaji mengineyo wapendayo.Mbali na huduma hiyo ya viwanja, Bayport ni taasisi ya kifedha inayojihusisha na mambo ya mikopo ya fedha, mikopo ya bidhaa bila kusahau bima ya elimu kwa uwapendao, huku huduma zote hizo zikifanikisha maisha bora kwa wateja wao na Watanzania kwa ujumla.
Meneja
Biashara wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Thabit
Mndeme, kushoto, akizungumza jambo wakati akitangaza taasisi yao
kuendelea kutoa huduma ya mradi wa viwanja vya Vikuruti, wilayani
Kibaha, mkoani Pwani, ulioanza Mei 22, mwaka huu na kupokewa vizuri na
Watanzania wengi. Kulia ni IT Meneja wa Taasisi hiyo, Daud Mavule.
“Bayport Financial Services ni taasisi yenye kutoa huduma bora kwa wateja wetu na Watanzania kwa ujumla, hivyo tunaamini huduma yetu ya mikopo ya viwanja kuwa endelevu ni sehemu ya kuhakikisha kwamba watu wote wanakuwa na uwezo wa kumiliki ardhi kwa ajili ya matumizi yao mbalimbali.
“Hii
ni huduma endelevu na muhimu inayotolewa kwa watu wote katika Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, ambapo mteja kutoka mahali popote anaweza
kumiliki kiwanja hicho kwa kuchukua fomu za kuomba viwanja hivyo kupitia
ofisi zetu zilizoenea nchi nzima, bila kusahau kwa wakala wetu Bank Of
Africa (BOA),” alisema.
Mndeme alisema kwamba sasa wateja wao watazidi kunufaika kununua viwanja vilivyopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, huku wakivipata kwa njia ya mkopo au kwa fedha taslimu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...