Ujumbe
wa Mfuko wa GEPF nchini Tanzania na Mwenyekiti wa Watanzania waishio
nchini Botswana wakiongozwa na Meneja Mahusiano wa Benki ya FNB
Botswana, Bibi Patricia Mpelega (wa pili kushoto) wakati wakielekea
kwenye tawi (Branch) la benki hiyo kwaajili ya uzinduzi wa akaunti
maalum ya kuwasilisha michango kwa Watanzania wainshio nchini humo, kwa
kujiwekea akiba zao za baadae.
Mkuu
wa Kitengo cha Masoko kutoka Mfuko wa GEPF, Aloyce Ntukamazina (wa tatu
kulia) akimpa maelezo mafupi juu ya mpango huo wa GDS Meneja Mahusiano
wa Benki ya FNB Botswana, Patricia Mpelega, muda mfupi kabla ya kuzindua
akaunti maalum.Wengine pichani ni Mwenyekiti wa watanzania waishio Botswana, Nieman Kissasi (kulia) na Meneja wa Mkoa wa Ilala Bw Jafari Meraji .

Bi
Patricia Mpelega akimpongeza Mwenyekiti wa watanzania waishio Botswana, Nieman Kissasi baada ya kukamilisha zoezi la ufunguzi rasmi wa akaunti ya Diaspora
Botswana

Mwenyekiti
wa Watanzania waishio Botswana Bw Nieman Kissasi akikamilisha utaratibu
wa kuwasilisha michango yake kama ishara ya uzinduzi rasmi wa akaunti
hiyo kulia kwake ni Meneja wa Mkoa wa Ilala Bw Jafari Meraji .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...