Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel leo imezindua promosheni kwa
wateja wake yenye lengo la kuboresha uhusiano pamoja na kuwazawadia
wateja wake nchi nzima kila wiki kwa muda wa siku 120.
Promosheni hiyo ijulikananyo kama " Jiongeze na Mshiko" ni ya kipekee
kwani inampatia mteja kujiunga na kushiriki bure kwa kujibu maswali na
kujishinda shilingi milioni 1 kila wiki na mwisho wa promosheni
kujishindia shilingi milioni 2. Na ikiwa mteja atapenda kujishindia
zawadi kubwa zaidi ataweza kujiunga na ngazi ya Premium kwa
kuchajiwa shilingi 300 kwa siku na kupata nafasi ya kujishindia
shilingi milion 3 kila wiki na mwisho wa promosheni kujishindia
shilingi milioni 50.
Akiongea wakati wa Uzinduzi wa promosheni hiyo, Meneja huduma za ziada
wa Airtel, Bi Prisca Tembo, alisema" promosheni hii inathihirisha
lengo letu la kuwawezesha watanzania kufikia ndoto zao na huku
tukiendelea kutoa huduma bora za kibunifu zinazokithi mahitaji yao.
Promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" itawawezesha watanzania wengi
kujishindia mamilioni ya pesa kila wiki na kuwawezesha kupata fedha
kwaajili ya kuendesha shughuli zao za kijamii na kiuchumi pindi
watakapoibuka washindi kwa muda wa wote wa mienzi minne.
Mteja atatakiwa kujibu maswali na kujikusanyia pointi
zitakazomwongezea nafasi ya ushindi na kuweza kujishindia zawadi ya
pesa taslimia kupitia promosheni hii ya " Jiongeze na Mshiko" natoa
wito kwa watanzania kujiunga na kupata nafasi ya kujishidia pesa
taslimu kila wiki.
Akiongea jinsi ya kujiunga na kushiriki , Afisa Uhusiano wa Airtel,
Jane Matinde alisema "wateja wataweza kujinga na promosheni hii bure
kwa kutuma ujumbe wenye neno "BURE" kwenda namba 15470, na kisha
kuanza kupokea maswali kwenye simu zao na kujibu maswali bure bila
gharama yoyote na kujikusanyia pointi. Mteja atakapomaliza kujibu
maswali ya bure atapata ujumbe utakaomuuliza kama angependa kujiunga
na ngazi ya premier, ili kuwezeshwa kufunguliwa maswali zaidi na
kujikusanyia pointi nyingi kwa zawadi zenye thamani kubwa.
Aliongeza kwa kusema maswali yatakayoulizwa ni ya kawaida hivyo
tunategemea wateja wetu watafurahia kuyajibu na kupata nafasi ya
kujishindia shilingi milioni 108 ikiwa ni moja ya njia ya kuwazawadia
kwa kutumia huduma zetu.
Alitoa wito kwa Tanzania kuwa waangalifu na kuhakiki taarifa zozote
wanazopewa kuhusu Ushindi kwa kupiga 100, namba yetu ya huduma kwa
wateja.
Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kulia),
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati
wa uzinduzi wa promosheni mpya ya Airtel 'Jiongeze na Mshiko'
itakayomwezesha mteja wa mtandao huo kujishindia mamilioni ya pesa kwa
njia ya sms. Katikati ni Meneja wa Huduma za Ziada wa Airtel, Prisca
Tembo na Afisa Huduma za Ziada, Fabian Felician.
Meneja wa Huduma za Ziada wa Airtel, Prisca Tembo (katikati),
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati
wa uzinduzi wa promosheni mpya ya Airtel 'Jiongeze na Mshiko'
itakayomwezesha mteja wa mtandao huo kujishindia mamilioni ya pesa kwa
njia ya sms. Kushoto ni na Afisa Huduma za Ziada, Fabian Felician na
Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...