DAR ES SALAAM, Alhamisi 9 Julai 2015: Kampuni ya Bima ya Resolution leo hii imeaanda hafla ya
kufuturisha wateja wake katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Hafla
ilihudhuriwa na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Musa Bin Salum.
Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa kampuni hiyo ya bima
kushirikiana na wateja wake katika iftar kwa lengo la kuwaleta karibu wateja
wao na kuwashukuru kwa ushirikiano wa mwaka hadi mwaka.
"Tunawashukuru
sana kwa kuhudhuria hafla hii na tunawapongeza kwa uvumilivu wenu katika mwezi
huu mkuu wa Ramadhan.” Meneja Mkuu wa
Resolution Insurance nchini Tanzania, Bwana Oscar Osir alisema.
Katika
hafla hiyo Shiekh Mkuu aliwakumbusha waumini wote umuhimu wa mfungo wa mwezi
mtukufu wa Ramadhan.
“Ningependa
kuwahimiza Waislamu wenzangu kutia maanani amri wakati wa Mwezi Mtukufu.
Tuonesha upendo na uvumilivu kwa wote, kusameheana na kuwasaidia wale ambao
hawana uwezo wa kujisaidia” Sheikh Alhad
alisema.
"Tunashukuru
sana kwa ushirikiano wenu kwani ndiyo inatupa motisha ya kuendelea kuwapa
huduma bora zaidi. Katika shughuli za kuwapa Huduma zilizo bora zaidi na
zinazoweza kuwahudumia ukiwa hapa nchini na hata sehemu yeyote duniani. Ningependa
pia kuwahakikishia kuwa tutaendelea kuwapa bidhaa bora na kuwasikiliza ili
tutimize mahitaji yenu", alisema Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa
Resolution Insurance Bi Zuhura Muro.
Baadhi wa waumini wa dini ya kiislam wakimsikiliza mgeni rasmi Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam .
Meneja Mkuu wa Bima ya Resolution, Oscar Osir, akiwatambulisha wageni waliaalikwa wa dini ya kiislam waliojumuika na Bima ya Resolution katika futari iliyoandaliwa na Bima ya Resolution katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...