MKURUGENZI wa Biashara wa Kampuni ya simu ya Zantel ofisi ya Zanzibar, Mohammed Mussa akizungumza katika hafla ya kukabidhi misaada ya vyakula iliyotolewa na kampuni hiyo kwa wazee mbali mbali wa Zanzibar.
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto, Msham Juma Khamis akihutubia wazee mbali mbali waliokua katika hafla ya kukabidhiwa msaada wa vyakula vilivyotolewa na kampuni hiyo. Kulia Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya simu ya ZANTEL, Mohammed Mussa na kulia Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazee Zanzibar (JUWAZA), Mwadini Kutenga.
NAIBU Katibu Mkuu, Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii , Vijana , Wanawake na Watoto, Nd. Msham Juma Khamis akimkabidhi msaada , Pili Ahmada wakati wa makabidhiano ya msaada wa vyakula uliotolewa na Kampuni ya simu ya Zantel kwa wazee mbali mbali wa Zanzibar, kulia Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel Zanzibar, makabidhiano hayo yalifanyika jana Kibanda maiti.
MZEE Hussein Abdalla akipokea msaada wa vyakula kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii , Vijana , Wanawake na Watoto, Nd. Msham Juma Khamis , msaada huo ulitolewa na kampuni ya simu ya Zantel, kulia Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel Zanzibar, makabidhiano hayo yalifanyika jana Kibanda maiti. (Picha na Haroub Hussein).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...