Mfanyabiashara wa Kimataifa Abbas Maziku akiwa katika picha ya pamoja na Mfanyabiashara ambaye pia ni Bilionea kijana Barani Afrika, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji, 'MO' ambaye anafuata nyayo zake katika kufikia malengo yake kibiashara.
Na Mwandishi Wetu
BIASHARA ya kusafirisha mazao ni miongoni mwa biashara zenye ushindani mkubwa kutokana na kutawaliwa na matajiri wenye asili ya Kiasia.
Kutokana na sababu hiyo imewafanya waafrika wengi kuwa na uthubutu katika biashara kwa kuhofia huenda wasifanikiwe na kujitanua kibiashara.
Mbali na ugumu huo lakini pia waafrika wengi hasa watanzania wamejikuta wakiishia kuwa wafanyabiashara ya kawaida na kupoteza fursa za kimataifa .
Kupoteza fursa muhimu za kimataifa kumefanya wakose fursa ambazo zingeweza kuwafanya wawe na mawazo mengine ya kuchangamkia fursa za kibiashara na kufikiri nje ya boksi.
Makala haya ndani ya mtandao huu yanaangazia mahojiano na mfanyabiashara wa kwanza wa kitanzania kufanya biashara ya kusafirisha Korosho kwenda nchini Vietnam aitwaye Abbas Maziku ambapo alielezea alipoanzia, vikwazo, mafanikio na matarajio yake kibiashara.
You look young and determined. Keep doing what you are doing. Sometimes taking tough initiatives in life, is the most funniest thing in human lifetime. Bravo young mana
ReplyDelete