Na Mwandishi Wetu
TAMASHA la manunuzi maarufu kama Pop Up Bongo, ambalo limeandaliwa na kampuni ya Studiored PR linatarajiwa kufanyika Jumamosi (Agosti 29) katika baa ya Triniti iliyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8 mchana hadi 2 usiku.
Tamasha hilo linalodhaminiwa na kampuni ya Smirnoff, ni la kwanza na la aina yake kufanyika jijini ambapo linafungua duka la muda mfupi la manunuzi ya rejareja ambapo wanunuaji watapata fursa kwa siku moja tu katika eneo maalum.
Maduka ya Pop Up duniani kote yanafanya mauzo ya rejareja kwa kuwapa wateja uzoefu wa manunuzi mbadala na wa ubunifu ambao ni tofauti kwa maduka ya rejareja yaliyozoeleka.
Aidha, bidhaa zitakazouzwa zitaleta shamrashamra nyingi, ufahamu na kuwapa wateja msisimko wenye furaha na wa kipekee kufanya manunuzi. Tamasha hilo linafanyika kila baada ya miezi mitatu hadi minne katika maeneo mbalimbali huku bidhaa mpya zikiuzwa katika kila tukio.
Hii ni fursa kwa ajili ya wajasiriamali wa ndani kuweza kutangaza bidhaa zao na kuweza kujulikana huku sekta ya fasheni na mtindo wa maisha ikizidi kukua.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...