Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel imeeandaa na kuendesha program maalum inayowawezesha watoto wa wafanyakazi wao kutembelea ofisi za Airtel na kupata wakati wa kujifunza na kuona mambo mbalimbali yanayofanywa na wazazi wao wakiwa ofisini kila siku. 
 Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Rasilimali watu Patrick Foya alisema”Wakati ni sasa kuwafunza watoto mambo mbalimbali yanayoendana na tecknologia ya karne hii, tunaamini ni muhimu kuwafunza kwa vitendo watoto wetu mambo wanayojifunza darasani au kuyasikia hasa kuhusiana na swala la mawasiliano, lengo nikuhamasisha watoto kuziunganisha na ndoto zao na kila mmoja kufikiria anataka kuwa nani katika maisha ya kesho. Program hii tumekuwa tukiifanya kila mwaka kwa kuwapa nafasi zaidi watoto wa wafanyakazi wa Airtel kwakutembelea ofisi zetu na kujionea mambo mbalimbali katika vitengo vyote. 
 Sambamba na hilo program hii imelenga kuunganisha familia kwani tunaamini wazazi wanatumia muda mwingi wakiwa kazini hivyo ni muhimu kwa watoto kujua wazazi wao walipo na wanachokifanya kwa manufaa ya taifa na familia kwa ujumla. Tunatambua tunao watoto wengi wenye ndoto za kuwa wahasibu, wahandisi, na na fani nyingine nyingi kwa kutembelea ofisi zetu tunaamini tutaweza kuonyesha namna gani wanaweza kuishi ndani ya ndoto hizo au kutimiza ndoto zao hapo baadae. Kwa upande wake mmoja ya wafanyakazi wa Airtel alisema “ Tunapata nafasi ya kuwaleta watoto wetu kila mwaka kwa umri tofauti tofauti , na kwakufanya hivi kumeniwezesha watoto wangu kujua ofisini kwangu, rafiki zangu na wafanyakazi wenzangu lakini pia wameweza kujua huku kazini huwa tunafanya kazi gani. 
 Program hii huwa inasubiriwa sana kwa hamu kila mwaka na watoto wamekuwa wakiifurahia sana kwani zimekuwa zinawaunganisha pia wao na watoto wengine na kujikuta wanajitengenezea marafiki na kujifunza toka kwa watoto wengine. Nawapongeza sana kitengo cha Airtel rasilimali watu kwa kutujali na kujali familia zetu kwa ujumla kwani program hii imeleta mwanga kwa watoto wetu kuhusisha wanachojifunza na wanachokiona katika idara mbalimbali. 
 Akiongea wakati wa maojiona na waandishi wa habari Vanessa Alisema nafurahi kuja Airtel kwani nimezoea kuona jengo kwa nje ni raha ukiwa humu ndani ya boti Huu ni mwaka wa 3 mfululizo Airtel inaendesha hii program yenye lengo la kuwapatia watoto mafunzo na kuwaleta karibu na wazazi wao.
 Afisa Rasilimali wa watu, Mubaraka Kibarabara (wa tatu kushoto), akiwafunza watoto ,wakati wa program maalum ya Airtel inayowawezesha watoto wa wafanyakazi wao kutembelea ofisi za Airtel na kupata wakati wa kujifunza
na kuona  mambo mbalimbali yanayofanywa na wazazi wao wakiwa ofisini kila
siku.
 Mkurugenzi wa mtandao wa Airtel Tanzania, Franky Filman,
akimfundisha motto jinsi ya kutumia mashine ya kutoa copy wakati wa  program maalum ya Airtel inayowawezesha watoto wa wafanyakazi wao kutembelea ofisi za Airtel na kupata wakati wa kujifunza na kuona  mambo mbalimbali yanayofanywa na wazazi wao wakiwa ofisini kila siku.
 Afisa Rasilimali wa watu, Mubaraka Kibarabara akiongea na mwandishi wakati wa  program maalum ya Airtel inayowawezesha watoto wa wafanyakazi wao kutembelea ofisi za Airtel na kupata wakati wa kujifunza na kuona  mambo mbalimbali yanayofanywa na wazazi wao wakiwa ofisini kila siku.
 Zoeylina Mabere akiongea na mwandishi wakati wa  program maalum ya Airtel inayowawezesha watoto wa wafanyakazi wao kutembelea ofisi za Airtel na kupata wakati wa kujifunza na kuona  mambo mbalimbali yanayofanywa na wazazi wao wakiwa ofisini kila siku.
Secelela Ngadada akiongea na mwandishi wakati wa  program maalum ya Airtel inayowawezesha watoto wa wafanyakazi wao kutembelea ofisi za Airtel na kupata wakati wa kujifunza na kuona  mambo mbalimbali yanayofanywa na wazazi wao wakiwa ofisini kila siku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...