Wakazi wawili wa Tabora na Musoma wameeleza
furaha yao mara baada ya Kampuni ya mawasiliano ya Airtel kuendelea
kukonga nyoyo za wateja wake na Watanzania kwa ujumla kwa kuwatangaza
na kuwakabithi pesa zao baada ya kuibuka washindi wa wiki ya pili ya
promosheni inayoendelea ya “Jiongeze na Mshiko”.
Washindi hao ni pamoja na , Gabriel Fernandis(18) mwanafunzi na mkazi
wa wa Mkoa wa Musoma mkoani Mara, yeye amejishindi shilingi milioni 1
, na mshindi wa pili ni Hamis Rashid(52)na mkazi wa Sikonge mkoa
waTabora yeye amejishindi shilingi milioni 3.
Sambamba na kukabithi zawadi hizo , Airtel imeendesha droo ya wiki ya
tatu ya “Jiongeze na Mshiko” katika ofisi ya makao makuu ya kampuni ya
Airtel iliyopo Morocco jijini Dar Es Salaam ilihudhuriwa na waandishi
wa habari na wasimamizi kutoka bodi ya bahati nasibu Tanzania.
Akiongea mara baada ya kukabithiwa zawadi yake , Grabriel Fernandisi
alisema”nimefurahi sana kuibuka mshindi katika promoshenii hii ambayo
nimeshiriki bure , bila gharama yoyote na kujibu maswali na
kujiongezea points zilizoniwezesha kushinda.
Nafurahia ushindi huu
kwasababu pesa hizi zitanisaidia kujiendeleza kwenye masomo yangu”
Akiongea na waandishi wa habari, Afisa uhusiano na matukio wa Airtel,
Dangio Kaniki, amesema kwamba tunayofuraha kuwazawadia washindi wa
wiki ya kwanza na ya pili ya promosheni “Jiongeze na Mshiko” ni
matumaini yetu kuwa pesa hizi zitawawezesha kuendesha shughuli zao za
kijamii na kiuchumi nakutatua changamoto mbalimbali wanazokumbana
nazo.
![]() |
Hamisi Rashid (kulia) mkulima wa Sikonge, Tabora akikabidhiwa fedha na Meneja wa Airtel Tabora, Phidelis Lugangila (Kushoto) baada ya kuibuka mshindi wa droo ya pili ya shindano la “Jiongeze na Mshiko”. |
Tutaendelea kuwazawadia wateja wetu kila wiki kwa muda wa wiki
16 hivyo natoa wito kwa watanzania kuendelea kujiunga na kushiriki
katika promosheni hii bila gharama yoyote na kupata nafasi ya
kujishindia.
Pamoja na kuwazawadia wateja wetu, leo pia tunaendesha droo ya wiki ya
tatu na kutangaza washindi wengine wawili ambao wameibuka washindi.
Katika droo ya leo tumebahatika kuwapata washindi wawili ambao ni
pamoja na Afrillious Kapinaa (21) mwanafunzi, Mkazi wa Dar es Saalam
amejishindia shilingi milioni moja pamoja na Shangai Rodger (53)
mfanyakazi wa TRA na mkazi wa Tanga amejishindia shilingi milioni 3"
“Tunawashukuru wateja wetu na Watanzania wote walioshiriki na wenye
sifa za kushiriki katika promosheni hii ya aina yake waendelee
kushirikiIli kwa kutuma ujumbe wenye neno “BURE” kwenda namba 15470,
na kisha kuanza kupokea maswali kwenye simu zao na kujibu maswali bure
bila gharama yoyote na kujikusanyia pointi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...