Airtel Tanzania imetanga washindi  wa droo yake ya nne ya promosheni  ya "Jiongeze na Mshiko"  katika ofisi za makao makuu ya Airtel zilipo Morocco jijini Dar Es Salaam, ambapo wateja wanaweza kushinda zawadi ya fedha kila wiki ya shilingi tatu , milioni  moja na mwisho wa promosheni mteja ataweza kuondoka na kitita cha shilingi milioni 50.

Akiongea wakati wa droo hiyo, Afisa uhusiano na matukio wa Airtel  Dangio Kaniki alisema leo tunatangaza washindi wawili wa  promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo watajishindia pesa taslim shilling milioni tatu na milioni moja kila mmoja. Ninayo furaha kutangaza washindi hao ambao  ni  Josephat Mahinda(25) Askari Magereza wa wa Mkoa wa Manyara yeye amejishindi shilingi milioni 3 , na  mshindi wa pili ni Daudi Ally Kingonji (31) mfanya biashara  na mkazi wa Kiwalani Dar Es Salaam yeye amejishindi shilingi milioni 1.”

Kaniki aliongeza kwa kusema, mpaka sasa Airtel imeshakabidhi zawadi kwa washindi mbali mbali hapa nchini. Na leo hii tumewakabidhi washindi wa droo ya tatu  ambao ni Shangai Rodger (53) mkazi wa Tanga yeye amejishindi shilingi milioni 3 , na  mshindi wa pili ni Afrillious Kapinaa  (21) mwanafunzi na mkazi wa mkoa wa Dar Es Salaam yeye amejishindi shilingi milioni 1 waliopokea zawadi zao leo  hii asubuhi.

Akiongea na waandishi wa habari Afrillious Kapinaa mwenye umri wa miaka 12, aliishukuru Airtel kwa kuanzisha promsheni hii. Ushindi wake ulikuja kama bahati na msaada mkubwa sana katika maisha yake ya uanafunzi. “Wazazi wangu wako Songea, ushindi huu wa milioni moja utanisaidia kutimiza mahitaji  yangu nikiwa hapa chuoni. Nawahimiza Wateja wengine wa Airtel kujiunga na prmosheni hii kwani ya ukweli kabisa”.

"Tunawashukuru wateja wetu na watanzania wote walioshiriki mpaka sasa katika promosheni hii. "Tunaamini ushindi huu utawawezesha wateja wetu kupata fedha za kuendesha shughuli zao za kiuchumi na kuboresha maisha yao, hilo ndilo lenge letu kama Airtel.  Natoa wito kwa watanzania kujiunga na kushiriki bure kwa kutuma ujumbe wenye neno BURE kwenda namba 15470 na kupata nafasi ya kushindia kupitia droo zetu za kila wiki." alimalizia Kaniki.
Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (katikati) akiwasiliana na mmoja wa washindi wakati wa kuchezesha droo ya nne ya promosheni ya Airtel "Jiongeze na Mshiko" iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambapo wateja wawili, Daudi Kingonji wa Dar na Josephat Mahinda wa Manyara waliibuka washindi. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Majjid Bakary na Afisa Huduma za Ziada wa Airtel, Fabian Felician.
Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kulia) akikabidhi zawadi ya kitita cha shilingi milioni 1, kwa mshindi wa droo ya tatu ya promosheni ya Airtel "Jiongeze na Mshiko", Agricius Kapinda katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (katikati) ni Afisa Huduma za Ziada wa Airtel, Fabian Felician.
Meneja mauzo wa Airtel Tanga Aluta Kweka (kulia) akikabidhi zawadi ya kitita cha shilingi milioni 3, kwa mshindi wa droo ya tatu ya promosheni ya Airtel "Jiongeze na Mshiko" Shangai Rodger, katika hafla iliyofanyika jijini Tanga jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...