Na Lorietha Laurence-Maelezo
Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini(RFB) imefanikiwa kufanya maboresho ya
barabara kwa kiwango cha lami katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa
Serikali ya awamu ya nne wa Mhe. Jakaya Kikwete.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Jana Bw. Joseph Haule
amesema kuwa matengenezo hayo yamefanikisha ujenzi wa barabara kuu
zinazounganisha mikoa mbalimbali nchini kukamilika kwa asilimia 89 huku zile za
Wilaya na Miji kwa asilimia 57.
“ kazi kubwa ya Mfuko huu ni kukusanya mapato kupitia vyanzo mbalimbali
ikiwemo tozo za barabarani na ushuru wa mafuta na baadaye kuzigawa kupitia
taasisi zinazohusika na ujenzi wa barabara ikiwemo TANROADS, Wizara ya
Ujenzi na Ofisi ya Waziri Mkuu “ alisema Bw. Haule
Aidha aliongeza kuwa Mfuko huo umefanikisha ujenzi wa daraja la Mabatini
jijini Mwanza ,daraja la Mwanhunzi na daraja la Mbutu linalounganisha Igunga
na Shinyanga pamoja na ununuzi wa vivuko kikiwemo kile cha Mv Malagarasi.
Mbali na hayo Bw.Haule aliongeza kuwa Bodi hiyo inaendelea kuhakikisha
barabara zinatunzwa kwa kudhibiti magari ya mizigo yanayozidisha uzito
unaochangia uharibifu wa barabara kwa kuanzisha mfumo wa kisasa wa kamera
utakaokuwa unaratibiwa na mfuko huo.
Mfuko huo umefanikiwa kuanzisha ujenzi wa barabara kwa kutumia mawe
ambao ni wa gharama nafuu na wa kudumu kwa muda mrefu,hata hivyo miradi
hiyo imeanza kutekeleza katika mikoa ya Kigoma na Mwanza.
Kutokana na mtandao wa barabara kufanyiwa matengenezo ya mara kwa mara
imesaidia kuongeza ubora wa barabara na kupanua wigo wa biashara kati ya
Tanzania na nchi za jirani ikiwemo Zambia,Malawi,Burundi,Rwanda na Uganda.
Mbali na mafanikio hayo Mfuko huounakabiliana na changamoto mbalimbali
ikiwemo upungufu wa bajeti kutokana na fedha zinazopatikana kutokukidhi
mahitaji.
Kazi nzuri mwenye macho aambiwi tazama
ReplyDelete