Mkurugenzi  wa kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Tanzania
Beatrice Singano, akiongea  na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi
wa ofa ya "Kamata Tano Zaidi" inayowawezesha wateja wa Airtel kupata
mara tano ya muda wa maongezi.



-Wateja kupata Bonus ya mara tano zaidi kwa kununua muda wa maongezi 
au kifurushi cha yatosha kupitia Airtel Money
-Wateja wote  wa malipo ya awali kufaidika

Dar es Salaam, Jumatatu Agosti 17, 2015, Kampuni ya simu za mikononi
ya Airtel leo imezindua ofa kabambe kwa wateja wake wa Airtel Money
ijulikanayo kwa jina la "Kamata tano Zaidi" itakayowawezesha wateja wa
Airtel kupata muda wa maongezi mara 5 zaidi pindi watakaponunua muda
wa maongezi au yatosha zaidi kupitia Airtel Money.

Akizungumza katika uzinduzi, Ofisa Mkuu wa Biashara wa Airtel ,
Arindam Chakrabarty alisema, kuanzishwa kwa bonus ya mara 5 zaidi  kwa
kununua muda wa maongezi kupitia Airtel Money ni katika juhudi za
Airtel  kuendeleza dhamira na azma yao ya kuwajali na kuwazawadia
wateja .

 "Lengo letu ni kutoa huduma nafuu, zenye ubora, tija na
zinazokidhi mahitaji ya mawasiliano kwa wateja wetu nchini kote. Nina
imani "Kamata Tano Zaidi" italeta uhuru wa kuwawezesha wateja wetu
kuwasiliana na familia zao,marafiki na hasa kuongeza ufanisi katika
biashara zao popote pale walipo . "

"Chakrabarty aliongeza kwa kusema, " tunawaahidi wateja wetu kupitia
huduma ya Airtel Money tutaendelea kuwapa huduma za kisasa na
kuwazawadia mara 5 ya matumizi yao kama bonus ya muda wa maongezi
itakayowawezesha kupiga simu kwenda namba yoyote ya Airtel kwa siku
hiyo".

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa AirtelTanzania, Beatrice
Singano, alisema, "Bonus ya mara 5 zaidi itapatikana kwenye aina zote
za manunuzi ya  muda wa maongezi yatakayonunuliwa  kwenye mfumo wa
Airtel Money kwa kupiga *150*60# na kuchagua namba 2. 

Muda wa maongezi 
utakaonunuliwa utajumlisha muda wa maongezi wa kawaida pamoja na 
vifurushi vyote vya Yatosha au Yatosha Noma. Bonus  ya mara 5 zaidi ya 
"Kamata Tano Zaidi" inayopatikana kwa kununua kupitia Airtel Money 
itadumu kwa muda wa masaa 24 toka muda uliponunuliwa, ili kuwatimizia 
wateja wetu mahitaji yao ya  mawasiliano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...