Mtaalam wa Misitu ambae pia anafanya kazi na  Mama Misitu kupitia Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF), Cassian Sanga akiendesha mjadala wa mada ya kwanza ya usimamizi  endelevu wa rasilimali za misitu nchini.
******************
Na Father Kidevu Blog.

 Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (MJUMITA)  leo imeanza mkutano wake Mkuu wa Siku mbili ambao kwanza umeanza na Warsha ya siku moja ya wadau wote wa mtandao huo. Wajum,be na wadau wa Mjumita kesho Agosti 18, watafanya mkutano mkuu ambapo mambo mbalimbali yatajadiliwa huku Kauli mbiu ya mwaka huu katika Mkutano huo unaofanyika mkoani Morogoro ikiwa ni 'TUCHAGUE VIONGOZI WATAKAO TETEA USIMAMIZI ENDELEVU WA MISITU".

Mtandao huo umeandaa rasimu maalum ambayo wanakusudia kuigawa kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuwa katika mikutano yao ya kampenzi itakayoanza Agosti 22 mwaka huu nchini kote wananchi wasisite kuwauliza wagombea hao juu ya mstakabali wa rasilimali za misitu zilizopo katika maeneo yao  kwa kuzingatia kuwa misitu ni uhai kwa maisha ya mwanadamu.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...