* Wateja kupata Bonus ya mara tano zaidi kwa kununua muda wa maongezi
au kifurushi cha yatosha kupitia Airtel Money
* Wateja wote wa malipo ya awali kufaidika
Kampuni ya simu za mikononi
ya Airtel leo imezindua ofa kabambe kwa wateja wake wa Airtel Money
ijulikanayo kwa jina la "Kamata tano Zaidi" itakayowawezesha wateja wa
Airtel kupata muda wa maongezi mara 5 zaidi pindi watakaponunua muda
wa maongezi au yatosha zaidi kupitia Airtel Money.
Akizungumza katika uzinduzi, Ofisa Mkuu wa Biashara wa Airtel ,
Arindam Chakrabarty alisema, kuanzishwa kwa bonus ya mara 5 zaidi kwa
kununua muda wa maongezi kupitia Airtel Money ni katika juhudi za
Airtel kuendeleza dhamira na azma yao ya kuwajali na kuwazawadia
wateja . "Lengo letu ni kutoa huduma nafuu, zenye ubora, tija na
zinazokidhi mahitaji ya mawasiliano kwa wateja wetu nchini kote. Nina
imani "Kamata Tano Zaidi" italeta uhuru wa kuwawezesha wateja wetu
kuwasiliana na familia zao,marafiki na hasa kuongeza ufanisi katika
biashara zao popote pale walipo . "
"Chakrabarty aliongeza kwa kusema, " tunawaahidi wateja wetu kupitia
huduma ya Airtel Money tutaendelea kuwapa huduma za kisasa na
kuwazawadia mara 5 ya matumizi yao kama bonus ya muda wa maongezi
itakayowawezesha kupiga simu kwenda namba yoyote ya Airtel kwa siku
hiyo".
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa AirtelTanzania, Beatrice
Singano, alisema, "Bonus ya mara 5 zaidi itapatikana kwenye aina zote
za manunuzi ya muda wa maongezi yatakayonunuliwa kwenye mfumo wa
Airtel Money kwa kupiga *150*60# na kuchagua namba 2. Muda wa maongezi
utakaonunuliwa utajumlisha muda wa maongezi wa kawaida pamoja na
vifurushi vyote vya Yatosha au Yatosha Noma. Bonus ya mara 5 zaidi ya
"Kamata Tano Zaidi" inayopatikana kwa kununua kupitia Airtel Money
itadumu kwa muda wa masaa 24 toka muda uliponunuliwa, ili kuwatimizia
wateja wetu mahitaji yao ya mawasiliano
Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano, akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofa ya "Kamata Tano Zaidi" inayowawezesha wateja wa Airtel kupata mara tano ya muda wa maongezi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...