MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Masha Mshomba, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya Mfuko huo barabara ya Bagamoyyo jijini Dar es Salaam, Agosti 16, 2015. Mfuko huo ulioanzishwa kwa sheria ya bunge namba 20 kifungu cha 5 ya mwaka 2008, una madhumuni ya kutoa fidia kwa Wafanyakazi kutokana na ulemavu au vifo viinavyosababishwa na ajali au magonjwa yatokanayo na kazi sambamba na kukuza mbinu za kuzuia matukio ya ajali, alisema. (Picha na K-VIS MEDIA)

Mfuko huo ambao umeanza kazi rasmi Julai 1, 2015, lengo kuu ni kutekeleza nia ya Serikali kukabiliana na changamoto za ulipaji wa fidia kwa Wafanyakazi katika mfumo wa utoaji fidia uliokuwepo awali, Mkurugenzi Mkuu Masha alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kiwango kidogo cha malipo ya fidia(kiwango kisichozidi shilingi 180,000) kwa ulemavu wa kudumu na shilingi 83,000 kwa wategemezi endapo kifo kitatokea kwa Mfanyakazi husika. Akinukuu sheria iliyoanzisha Mfuko huo, Masha alisema, kifungu cha pili (2), cha sheria ya fidia kwa wafanyakazi namba 20/2008 Mfuko huu unawahusu Waajiri na Wafanyakazi wote katika sekta ya Umma na Binafsi, Tanzania Bara pekee. "Naomba ieleweke, anayepaswa kuchangia kwa mujibu wa sheria hii ni Mwajiri na sio Mfanyakazi kukatwa mshahara wake." Alifafanua Masha
Waandishi wa Habari kazini
 Masha (katikati), akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa hifadhi za Jamii kutoka Wizara ya Kazi na Ajira, Daudi Kaali, (kulia) na Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera wa Mamlaka ya Kusimamia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini, SSRA, Ansgar Mushi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. shida ni kuzipata hizo hela za fidia pale unapokumbwa na matatizo yanahitaiji ulipwe fidia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...