Tanzania inaingia katika kipindi kigumu na cha muhimu sana kwenye historia yake. Ni kipindi ambacho kitasaidia kuamua muelekeo wa nchi kwa miaka mitano inayokuja. Mara nyingi ifikapo wakati wa uchaguzi kuna mambo mengi hubadilika. Biashara huanza kuwa ngumu kutokana na hofu miongoni mwa watu. Pia, ushiriki wa watu kwenye kampeni hufanya muda mwingi kutumika huko hivyo kutoa muda mchache kwenye shughuli kama kazi.
Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, mwaka huu tutashuhudia mabadiliko makubwa sana, mabadiliko haya siyo tu aina ya watu wanaoshiriki kwenye kugombea nafasi mbalimbali, bali pia mfumo utakaotumika kwenye kampeni hadi upigaji kura. Mwaka huu tutashuhudia matumizi ya Tehama kwa kiwango kikubwa sana kwenye kampeni za uchaguzi na hata utangazaji na uchungaji wa matokeo ya chaguzi.Tutegemee kupata updates za matokeo ya kura toka kila kituo ndani ya dakika punde tuu wanapomaliza kuhesabu.

Kwa chama chochote kinachotaka kufikia watu na hatimaye kushinda, ni ngumu kufanikisha hilo bila kutumia Tehama. kwa maneno mengine, Tehama ndiyo itakayoongoza uchaguzi wa mwaka huu. Tumeona mfano wa Obama mwaka 2008. Akiongozwa na kauli mbiu yake ya pamoja tunaweza (Yes we can) na matumizi ya mitandao, Obama aliweza kufikisha ujumbe kwa vijana wengi kama ilivyo sasa kwa Tanzania, na hatimaye kushinda uchaguzi wa kihistoria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...