Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Chama hicho kiko makini katika kumuengua Mwanachama wake ye yote anayetumia hila katika mchakato wa kutaka achaguliwe kuwa Kiongozi kupitia chama hicho.
Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na Vijana walioamua kutoka chama cha Upinzani na kujiunga na CCM ambapo wameanzisha Maskani iliyopewa jina la Balozi Seif Maskani hapo katika Kijiji cha Kinazini Mtambwe Kusini.
Balozi Seif ambae alipata wasaa wa kuikagua Maskani hiyo na kuahidi kusaidia ujenzi utakaolingana na hadhi ya Chama chenyewe alisema CCM kuendelea kukumbatia wala rushwa ni sawa na kwenda kinyume na Sera na Ilani yake.
Alisema maamuzi yaliyofanywa katika vikao mbali mbali vya Viongozi wa ngazi za juu ya Chama hicho kuwaengua wanachama waliotumia njia ya rushwa katika kusaka Uongozi yalikuwa sahihi na yanapaswa kuungwa mkono na Wanachama pamoja na wapenda haki wote Nchini.
Aliwatoa hofu wana CCM na Wananchi wote kwamba Chama cha Mapinduzi kimekuwa na utaratibu wa kuhusisha wanachama wake katika mchakato wa kuchaguwa Viongozi wake kwa kutumia mfumo wa Demokrasiaya wengi iliyokomaa.
Balozi Seif amewapongeza Vijana hao wa Kijiji cha Kinazini Mtambwe Kusini kwa uamuzi wao wa kujiunga na Chama cha Mapinduzi chenye Sera na Ilani inayotekelezeka.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM Taifa aliwaahidi Vijana hao kwamba CCM itawapa neema kwa kuwasimamia kutatua changamoto zinazowakabili katika harakati zao za kujitafutia maendeleo.
Balozi Seif Ali Iddi aliwaonya Viongozi na wanachama wa upinzani kusitisha tabia ya kumzushia pamoja na kumsakama bila ya sababu za msingi kwa mambo ambayo hajayafanya.
Kijana Ali Abdulla Bakari wa Balozi Seif Maskani ya kijiji cha Kinazini Mtambwe Kusini akieleza changamoto zinazowakabili wakati Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif alipofanya ziara ya kuwatembelea baada ya uamuzi wao wa kujiunga na CCM na kuachana na upinzani.
Balozi Seif akizungumza na Wana CCM na wanamaskani wa Balozi Seif wa Kinazini Mtambwe na kuahidi kwamba CCM inasaidia ujenzi wa Jengo la Maskani yao waliyoianzisha.
Balozi Seif akimkabidhi mchango wa shilingi Milioni 1,000,000/- Katibu wa Maskani ya Balozi Seif ya Kijiji cha Kinazini Mtambwe ili kuanzia msingi wa Jengo lao la Maskani.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa CCM Balozi Seif akibadilishana mawazo na Vijana wa Maskani ya Maida Mtambwe baada ya kuwasalimia kwa muda mfupi alipokuwa katika ziara ya Mkoa Kaskazini Pemba. Picha na OMPR – ZNZ.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...