Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema kwamba wakati Serikali inaendelea na jitihada za kuimarisha sekta ya Kilimo ili ikue kwa kasi ya asilimia Tano Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wanapaswa kuitumia fursa ya uzalishaji wa mazao ya Kilimo kuwekeza katika miundombinu na viwanda kwa lengo la kuyaongezea thamani mazao hayo. 
Alisema uwekezaji huo utawapa nguvu zaidi za uzalishaji wakulima na hatimae kuongeza kipato chao kutokana na uzalishaji wa bidhaa zilizo katika kiwango kinachokubalika Kimataifa na hivyo kupunguza umaskini kwa Wananchi nchini ambao wengi wanategemea sekta hiyo mama kuendesha maisha yao ya kila siku. Balozi Seif Ali Iddi alitoa rai hiyo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku Kuu Wakulima iliyoambatana na Maonyesho ya Wakulima Nane Nane Mwaka 2015 Kanda ya Mashariki yanayofanyika katika uwanja wa Taifa wa Mwalimu J.K. Nyerere uliopo Mkoani Morogoro. 
Alisema juhudi hizo za Serikali Kuu zimehusisha kuendeleza miundombinu ya umwagiliaji maji ili kuondokana na kilimo cha kutegemea mvua, kuondoa kodi katika zana mbali mbali za sekta ya kilimo sambamba na uimarishaji wa bara bara za vijijini ili kuongeza tija. 
Balozi Seif alisema Serikali imeamua kutekeleza Mpango wa matokeo Makubwa  sasa  kuanzia mwaka 2013/2014 ukilenga kuleta matokeo makubwa na ya haraka, ambapo Kilimo kikitegemewa kuwa miongoni mwa sekta sita zilizopewa kipaumbele kutekelezwa kwa mpango huo. 
Ujumbe wa maadhimisho ya siku kuu ya Wakulima Nane nane mwaka huu wa 2015 unasema ” Matokeo makubwa sasa { BRN } uchague Viongozi bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji “.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiingia katika eneo la Maonyesho ya Siku Kuu ya Wakulima Nane nane zilizoadhimishwa katika Uwanja wa Mwalimu J.K. Nyerere Kanda ya Mashariki uliopo Mkoani Morogoro akiwa na Viongozi wa Kanda hiyo.
 Luteni Mtui wa JKT akimfahamisha Balozi Seif hatua inayochukuliwa na Jeshi hilo katika kuimarisha kilimo cha mazao mbali mbali kwa kutumia Utaalamu wa
Kisasa.
 Mmoja wa Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar jitihada wanazochukuwa wakulima katika kuendesha kilimo kwa njia ya kisasa. Kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Tanzania
Bwana Salum Mwakuginda.
 Balozi Seif akiridhika na kazi kubwa inayoendelezwa na Shrika la Mzinga linalojishughulisha na utengenezaji wa samani za Majumbani na Ofisini na kushawishika kutajka kuweka oda ya ununuzi kwa ajili ya baadhi ya skuli za Jimbo lake

Watendaji wa Kampuni ya kigeni ya uuzaji wa vifaa vya Mtandao wa kisasa vya simu ya FFTG kutoka Nchini Jamuhuri ya Watu wa China nayo ni miongoni mwa taasisi zilizoshiriki maonyuesha ya wakulima Nane nane Mkoani Morogoro ambapo Balozi Seif alipata wasaa wa kuitembelea.
Balozi Seif akikabidhi Kikombe cha ushindi wa Pili wa Jumla kwenye maqonyesho na wakulima Nane nane Mjini Mrogoro uliochukuliwa na Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Tanzania Bwana Salum Mwakuginda na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadiq. Picha na OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...