![]() |
Kingunge Ngombale Mwiru |
Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM lililokutana tarehe 15.08.2015 katika ukumbi wa Julius Nyerere International convention centre, pamoja na mambo mengine liliazimia mambo yafutauo:-
1. Lilimvua Ukamanda
Mkuu ndugu Kingunge Ngombale Mwiru. Maamuzi hayo yalitolewa kutokana na
tabia na mwenendo wake wa hivi karibuni kuenda tofauti na maadili na
taratibu za CCM.
Aidha kikao kimetoa
mapendekezo kwa vikao vya Chama Cha Mapinduzi kuuangangalia upya
uanachama wake na kuchukua hatua kubwa zaidi.
2. Kikao pia kiliunda
timu ya kampeni ambayo itafanya kazi pamoja na kamati ya utekelezaji
kuhakisha ushindi wa CCM kwa nafasi zote.
3. Kikao kimemshukuru
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dr. Jakaya
Mrisho Kikwete kwa hotuba nzuri ya ufunguzi wa Baraza na kikao
kimeahidi kutekeleza maagizo na maelekezo ya hotuba hiyo kwa matendo.
Sixtus Raphael Mapunda
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa
Mzee hata wewe wamekumwaga basi Ukawa raundi hii utatumaliza
ReplyDeleteHawa vijana wakumbuke kama watu kama hawa walikibeba chama na kuongoza nchi tangu kabla ya kuzaliwa kwao.Baharia wanapoanza kutumbukiza manahodha baharini, kuna balaa kubwa laja.Mtoto asiyesikia la mzee.........
ReplyDelete