Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom imekanusha taarifa za uvumi zilizotangazwa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa inaendesha kampeni kupitia ujumbe mfupi wa maneno kumfanyia kampeni mgombea urais kupitia UKAWA.
Vyombo hivyo viliandika habari za uzushi kuwa Vodacom imeanzisha promosheni kupitia ujumbe mfupi wa maneno inayojulikana
kama “Jiunge na Lowassa” kitu ambacho hakipo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Rene Meza ameeleza kuwa kampeni zinazoendeshwa hivi sasa na Vodacom zinahusiana
na kuwaongezea muda wa maongezi na data wateja wake na haina kampeni nyingine yoyote.
“Katika
siku za karibuni tulizindua kampeni kwa ajili ya wateja wetu
zinazohusiana na kuwapatia wateja wetu ofa
ya muda wa maongezi na data hatuna kampeni zozote za kisiasa wala
hatujihusishi na kampeni za vyama vya siasa bali tupo kwa ajili ya
kuwahudumia watanzania wote na kuendelea kutoa huduma bora za
mawasiliano nchini kote”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...