BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) limeipongeza kampuni ya Compass Communications Tanzania kwa kufanya mashindano bora ya Miss Universe hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa mashindano ya Miss Universe Fausta Magoti wakati wa kufanya tathimini ya mashindano ya mwaka jana ambapo, Caroline Benard aliibuka mshindi.
Magoti alisema kuwa pamoja na kampuni ya Compass kuanza kushiriki katika mashindano ya Miss Universe mwaka 2007, waliweza kufanya vyema na kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake.
Mbali ya kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, Magoti alisema kuwa wameridhishwa sana na utendaji wa kamati hiyo kwa kuteua majaji ambao wamekuwa wakiwatangaza washindi ambao ni mfano bora kwa tabia kwa jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...