Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim Tanzania akizingumza na baadhi ya wafanyakazi pamoja na wateja wa benki hiyo wakati
wa hafla fupi iliyoaandaliwa na benki hiyo kuadhimisha miaka 18 tangu
kuanzishwa kwa benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika kwenye makao makuu ya
benki hiyo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa juma lililopita.
Baadhi ya wafanyakazi wa
Benki ya Exim Tanzania pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo
wakifurahia kwa pamoja wakati wa hafla fupi iliyoaandaliwa na benki
hiyo kuadhimisha miaka 18 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo. Hafla hiyo
ilifanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam,
mwishoni mwa juma lililopita
Meneja
Mwandamizi wa Benki ya Exim Tanzania tawi la Exim Tower, Bi Rose Kanijo
(wa tano kulia) akiwaongoza wawakilishi wa wateja wa benki hiyo Bw.
Geofrey Mihaambo (wan ne kulia) na Bi. Usha Kakad (wa tatu kulia) kukata
keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili maadhimisho ya miaka 18
tangu kuanzishwa kwa benki hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye makao
makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa juma
lililopita.Wanaoshuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
Meneja
Mwandamizi wa Benki ya Exim Tanzania tawi la Exim Tower, Bi Rose Kanijo
(wa tano kulia) akiwaongoza wawakilishi wa wateja wa benki hiyo Bw.
Geofrey Mihaambo (wan ne kulia) na Bi. Usha Kakad (wa tatu kulia) kukata
keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili maadhimisho ya miaka 18
tangu kuanzishwa kwa benki hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye makao
makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa juma
lililopita.Wanaoshuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
Exim
Bank imeadhimisha miaka 18 tangu kuanzishwa kwake huku uongozi wa benki
hiyo ukiahidi kuboresha zaidi huduma zake hasa katika kipindi hiki
ambacho sekta benki imetawaliwa na ushindani mkubwa.
Benki
hiyo iliyoanza kutoa huduma zake mwezi Agosti,1997 ikiwa na tawi moja
jijini Dar es Salaam kwa sasa ina jumla ya matawi 30 hapa nchini na
matawi saba nje ya nchi huku pia rasilimali yake ikitajwa kuwa na
thamani ya sh. trilioni 1.1 hadi kufikia mwezi juni mwaka huu.
Akizungumza
hivi karibuni kwenye hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo
jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha baadhi ya waafanyakazi na wateja
wa benki hiyo, Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw Selemani Ponda
alisema mafanikio hayo kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na ukweli kuwa
benki hiyo inafanya kazi chini ya bodi ya wakurugenzi iliyo imara.
“Siku
kama ya leo miaka 18 iliyopita ndio benki yetu ilianzishwa. Leo benki
ya Exim imesaidia ukuaji wa biashara ndani na nje ya nchi na
tunashukuru kuona kwamba baadhi ya wateja wetu wameweza kuhudhuria hafla
hii ili tusherehekee pamoja siku hii muhimu,’’ alisema.
Kwa
mujibu wa Bw. Selemani mbali ya kuwa na idadi kubwa ya matawi ndani na
nje ya nchi pia imefanikiwa kuwa na mashine za kutolea fedha 57 hapa
nchini, vituo vya mauzo zaidi 250 na kwa sasa ina matawi kwenye mikoa 16
hapa nchini ambayo yanahudumia takribani wateja 180,000.
“Miaka
yote tumekuwa tukiitumia siku hii pia kutathmini ubora wa huduma zetu
kwa wateja na ndio maana tumekuwa tukiendelea kufanya vizuri kila siku.
Uhodari wa wafanyakazi wetu imekuwa pia imekuwa ni chachu kwenye
mafanikio haya,’’ alibainisha bw. Ponda.
Kwa
mujibu wa Bw. Ponda, benki hiyo ndio benki ya kwanza hapa nchini
kufungua matawi yake nje nchi ambapo kwa sasa imefungua matawi yake
visiwa vya Comoro na nchini Djibouti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...