Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde, inaeleza kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi -CUF, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo mbele ya Waandishi wa habari kwenye `hoteli ya Peacock, Jijini Dar es salaam leo.

Prof. Lipumba amesema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kukiukwa kwa Katiba ya Chama chao.

TAARIFA KAMILI 

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

MWENYEKITI wa Taifa wa  Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho leo majira ya saa 5 asubuhi katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mbele ya waandishi habari,Pro.Lipumba amesema ametafakari sana katika kuendelea kuwa Mwenyekiti wa chama hicho lakini dhamira yake inamsuta.
Amesema kuwa mwaka 2014 hakutaka kugombea nafasi hiyo kutokana na mchakato wa katiba mpya akaamua kugombea kwa lengo ya kuwapa watanzania  katiba itakayoindoa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Lipumba amesema katika mchakato wa bunge maalumu wakaunda umoja wa katiba (UKAWA0 wenye lengo wa kusimamia katiba iliyopendekezwa lakini sasa waliopitisha ndio wanataka kuisimamia katiba hiyo ambayo haingii akilini.
Amesema alikuwa akishiriki vikao vya UKAWA lakini Aprili 1 mwaka huu alisema atang'atuka katika nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Wanannchi (CUF).
Amesema amepita katika misukosuko mingi katika kukijenga chama hadi kufikia kiasi hata kabambikiziwa  kesi ya kufanya maandamano bila kibali.

Lipumba amesema kazi yake atakuwa mwanachama wa kawaida, kufanya utafiti wa maendeleo endelevu  pamoja na kufanya ushauri wa masuala mbalimbali katika chama hicho.
Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba akizungumza na Wandishi wa habari katika moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Peacok hotel jijini Dar leo kuhusiana na kung'atuka kwake rasmi Uenyekiti wa chama hicho na kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida,ambapo Mh Lipumba ameeleza kuwa yeye atabaki kuwa mwanachama hai na halali wa kawaida kwa sababu kadi yake ya uanachama ameshailipia mpaka mwaka 2020 
 Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akiwa na wananchi wa kawaida kulia, Abdala Shabani  pamoja na mdogo wake,Shabaani Miraji wakiwa wamemsindikiza aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF taifa ili kuzungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wananchi katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa  mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akitangaza kujiuzulu wadhifa wake katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha rasimu  ya Katiba pendekezwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ndio iliyosababisha kuungana na kuunda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)  katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
 Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo katika mkutano wa kujivua uenyekiti wa chama cha CUF leo jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akikusanya makabrasha yake mara baada ya kumaliza mkutano wa kujivua uanachama wa chama cha CUF taifa katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Lidu alisema mjamaa akija atatuvuruga. Na kweli amewavuruga. Na bado tutasikia mengi mbeleni

    ReplyDelete
  2. Huo ndio msimamo wa uhakika na wakiume. Tunaakuunga mkono baba. Hivi hawa akina seif sharif wana akili?

    ReplyDelete
  3. ..HUYU Prof.Lipumba katuvunja moyo sana....Huu ni wakati wa Mabadiliko, kwanini anaondoka muda huu??? Haoni kuwa kwa kufanya hivyo anaiua pia ndoto yake ya KULETA MABADILIKO TANZANIA....Itabidi tujiulize hivi kweli Prof. Alikuwa muumini wa kweli wa Mabadiliko??? Nawasiwasi sana, huenda ikawa hakuwahi kuwa muumini wa mabadiliko....amekuwa anatulaghai muda wote huu....
    KILA LA KHERI HUKO UENDAKO PROF.Lipumba..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Somebody plse plse bring me another bag of popcorn, the nigerian movie is abt to start..... Kabla ya october tutaona mengi

      Delete
    2. Prof. Lipumba ni muumini wa kweli wa mabadiliko lkn kaingia fisadi kwenye umoja wa mabadiliko na kupokewa kinyume na katba ili tu watu flani wanufaike pamoja nae fisadi huyo kwaiyo mabadiliko hayatatokea chini ya huyo fisadi zaidi ya alie tajili atazidi kua tajiri na alie masiki ataendelea kua masikini zaidi yan kufa kabisa!!!

      Delete
  4. Haya akavae magwanda ya Kijani. .huo uenyekiti usiokuwa na mwisho siyo demokrasia. .hongera Dr. Kwa kusoma alama za nyakati..Damu mpya mawazo mapya na nguvu mpya vinahitajika

    ReplyDelete
  5. Lakini hajaondoka CUF
    Wala UKAWA
    Tusubiri
    October. Atakuwa nani ndani i ya UKAWA

    ReplyDelete

  6. KWELI TUTASIKIA MENGI, NA MENGI YANAKUJA

    ReplyDelete
  7. Tatizo la wanasiasa wa bongo ni kujali masilahi binafsi. Kama lengo la upinzani ni kuiondoa CCM madarakani basi kina Prof. Lipumba na wa aina yake hawana nafasi katika mageuzi kwani wanaendekeza masilahi binafsi badala ya umma. Kila la kheri Prof. Lipumba katika maisha ya siasa. Mbona ulishiriki kwa mbwembwe kumkaribisha Lowassa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sijui kwa nini? Ila nasikia kukereketwa kusikia kuwa lengo la ukawa ni kuiondoa CCM madaraka, that's rubbish. Ukawa hakuna malengo wanayoweza kuyasema kuvutia wapiga kura. Mi mtanzania nataka ajira, afya, elimu, usafiri mzuri, nifaidi rasilimali za nchi yangu. CCM ikiwa au isiwe madarakani inanisaidia nini. Nampa kura .mwenye sera zitazonifaa, sera ya nahakikisha naitoa CCM inaniudhi. Inanithibitishia kweli wana uroho wa madaraka na kukomoana na kulindana na hawana nia ya kumsaidia mnyonge.
      acheni hizo

      Delete
    2. nakuunga mkono mkuu, maslahi binafsi ndo tatizo kubwa kwa viongozi Tz plus ubinafsi!!

      Delete
  8. Fanyeni kazi za kuwaingizia mkate wenu wa kila siku acheni kuahangaika na siasa za Tanzania na Africa kwa ujumla. Tumeshao Afrika nzima siasa za vyama vingi ilikuwa bado, ndiyo maana kila kona watu wameuana, wamefungana,na kadha wa khadha. sisi Africa tutawaliwe Ki-sultani kama kwa Mswati au Chama kimoja maana kila mtu anakimbilia IKULU tu, wote mtaingia huko?. Vilio vya nani angie ikulu kila kona? ahaaa!!!! wanatuchanganya.

    ReplyDelete
  9. The mdudu, mbona sisi wakuona mbali tulishayajua haya mapema hivi tujiulize kweli binaadamu kwenye kuoga kuna ukomo jibu no lazima binaadamu yoyote yule mpenda usafi kuoga sio ombi bali lazima lakini hawa wame muogesha siku mbili tu tena kwa shangwe kubwa walipotaka kumuogesha tena mwezao kakataa katakata hapo ndipo kasheshe limefumuka nguzo muhimu hiyo imetoka ya kwanza na bado nguzo ya pili yaja wakati wowote swali je nyumba itasimama bila ya NGUZO? yangu macho si Ukawa wala CCM mimi ACT Wazalendo mwendo wa Nyerere chukua pesa za mapapa + za mafisadi sambaza kwa wanyonge.......mungu mkubwa huwezi kushinda na na mungu na bado mwendo mchibuyu

    ReplyDelete
  10. Kwa mtazamo wa haraka watanzania tumekuwa wagumu kupambanua mambo .tuingie kwa kina tutaelewa Prf Lipumba Dr Slaa hawa watu wana mawazo ya mbele Sana ambayo binadamu wa kawaida hawezi elewa .hv nyie inwaingia akilini mtu waliemuita mchafu Leo hii wanamkaribisha Na kumpa madaraka makubwa Ina maana ukawa asingepatikana lowasa wasingemsimamisha mgombea?

    ReplyDelete
  11. NI HERI LAWAMA KULIKO FEDHEHA. yaaani kwa nini uyalambe MATAPISHI YAKO MWENYEWE? huyu MZEE LOWASSA Hana AGENDA YA WATANZANIA Bali YAKE BINAFSI na Prof Lipumba KALIONA HIYO MAPEMA. MTU HUWEZI KUUNUNUA URAISI KWA BEI KUBWA KIASI HICHO. Utazidudishaje??? NA IKULU HAKUNA BIASHARA? JAMANI MBONA TUNAWEKA RASLIMALI YETU REHANI? lowassa ni wa kukimbiwa kama MLOZI. prof Lipumba ni uwamuzi wa KIJASIRI.

    ReplyDelete
  12. Hii ni kumalizana kisiasa, kupiganaa ngwala kisiasa, na kutojali michango ya wengine, ama kweli vyama vina wenyewe.

    ReplyDelete
  13. Movie ndo kwanza inaanza.Script imeshaandikwa kilichobaki ni maigizo tu.Kweli CCM imejipanga.Kidumu Chama Cha Mapinduzi.Idumu amani na maendeleo ya nchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...