Taarifa
iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde, inaeleza kuwa Mwenyekiti wa
Chama cha Wananchi -CUF, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba ametangaza
kujiuzulu wadhifa wake huo mbele ya Waandishi wa habari kwenye `hoteli
ya Peacock, Jijini Dar es salaam leo.
Prof. Lipumba amesema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kukiukwa kwa Katiba ya Chama chao.
TAARIFA KAMILI
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MWENYEKITI
wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa
Ibrahim Lipumba amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho leo majira ya saa
5 asubuhi katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mbele ya waandishi habari,Pro.Lipumba amesema ametafakari sana katika kuendelea kuwa Mwenyekiti wa chama hicho lakini dhamira yake inamsuta.
Amesema kuwa
mwaka 2014 hakutaka kugombea nafasi hiyo kutokana na mchakato wa katiba mpya
akaamua kugombea kwa lengo ya kuwapa watanzania
katiba itakayoindoa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Lipumba
amesema katika mchakato wa bunge maalumu wakaunda umoja wa katiba (UKAWA0 wenye lengo wa
kusimamia katiba iliyopendekezwa lakini sasa waliopitisha ndio wanataka
kuisimamia katiba hiyo ambayo haingii akilini.
Amesema
alikuwa akishiriki vikao vya UKAWA lakini Aprili 1 mwaka huu alisema atang'atuka
katika nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Wanannchi (CUF).
Amesema
amepita katika misukosuko mingi katika kukijenga chama hadi kufikia kiasi hata kabambikiziwa
kesi ya kufanya maandamano bila kibali.
Lipumba
amesema kazi yake atakuwa mwanachama wa kawaida, kufanya utafiti wa maendeleo
endelevu pamoja na kufanya ushauri wa
masuala mbalimbali katika chama hicho.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba akizungumza na Wandishi wa habari katika moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Peacok hotel jijini Dar leo kuhusiana na kung'atuka kwake rasmi Uenyekiti wa chama hicho na kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida,ambapo Mh Lipumba ameeleza kuwa yeye atabaki kuwa mwanachama hai na halali wa kawaida kwa sababu kadi yake ya uanachama ameshailipia mpaka mwaka 2020
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akiwa na wananchi wa kawaida kulia, Abdala Shabani pamoja na mdogo wake,Shabaani Miraji wakiwa wamemsindikiza aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF taifa ili kuzungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wananchi katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akitangaza kujiuzulu wadhifa wake katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha rasimu ya Katiba pendekezwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ndio iliyosababisha kuungana na kuunda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo katika mkutano wa kujivua uenyekiti wa chama cha CUF leo jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu
Lipumba akikusanya makabrasha yake mara baada ya kumaliza mkutano wa
kujivua uanachama wa chama cha CUF taifa katika ukumbi wa mikutano wa
hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Lidu alisema mjamaa akija atatuvuruga. Na kweli amewavuruga. Na bado tutasikia mengi mbeleni
ReplyDeleteHuo ndio msimamo wa uhakika na wakiume. Tunaakuunga mkono baba. Hivi hawa akina seif sharif wana akili?
ReplyDelete..HUYU Prof.Lipumba katuvunja moyo sana....Huu ni wakati wa Mabadiliko, kwanini anaondoka muda huu??? Haoni kuwa kwa kufanya hivyo anaiua pia ndoto yake ya KULETA MABADILIKO TANZANIA....Itabidi tujiulize hivi kweli Prof. Alikuwa muumini wa kweli wa Mabadiliko??? Nawasiwasi sana, huenda ikawa hakuwahi kuwa muumini wa mabadiliko....amekuwa anatulaghai muda wote huu....
ReplyDeleteKILA LA KHERI HUKO UENDAKO PROF.Lipumba..
Somebody plse plse bring me another bag of popcorn, the nigerian movie is abt to start..... Kabla ya october tutaona mengi
DeleteProf. Lipumba ni muumini wa kweli wa mabadiliko lkn kaingia fisadi kwenye umoja wa mabadiliko na kupokewa kinyume na katba ili tu watu flani wanufaike pamoja nae fisadi huyo kwaiyo mabadiliko hayatatokea chini ya huyo fisadi zaidi ya alie tajili atazidi kua tajiri na alie masiki ataendelea kua masikini zaidi yan kufa kabisa!!!
DeleteHaya akavae magwanda ya Kijani. .huo uenyekiti usiokuwa na mwisho siyo demokrasia. .hongera Dr. Kwa kusoma alama za nyakati..Damu mpya mawazo mapya na nguvu mpya vinahitajika
ReplyDeleteLakini hajaondoka CUF
ReplyDeleteWala UKAWA
Tusubiri
October. Atakuwa nani ndani i ya UKAWA
ReplyDeleteKWELI TUTASIKIA MENGI, NA MENGI YANAKUJA
Tatizo la wanasiasa wa bongo ni kujali masilahi binafsi. Kama lengo la upinzani ni kuiondoa CCM madarakani basi kina Prof. Lipumba na wa aina yake hawana nafasi katika mageuzi kwani wanaendekeza masilahi binafsi badala ya umma. Kila la kheri Prof. Lipumba katika maisha ya siasa. Mbona ulishiriki kwa mbwembwe kumkaribisha Lowassa?
ReplyDeleteSijui kwa nini? Ila nasikia kukereketwa kusikia kuwa lengo la ukawa ni kuiondoa CCM madaraka, that's rubbish. Ukawa hakuna malengo wanayoweza kuyasema kuvutia wapiga kura. Mi mtanzania nataka ajira, afya, elimu, usafiri mzuri, nifaidi rasilimali za nchi yangu. CCM ikiwa au isiwe madarakani inanisaidia nini. Nampa kura .mwenye sera zitazonifaa, sera ya nahakikisha naitoa CCM inaniudhi. Inanithibitishia kweli wana uroho wa madaraka na kukomoana na kulindana na hawana nia ya kumsaidia mnyonge.
Deleteacheni hizo
nakuunga mkono mkuu, maslahi binafsi ndo tatizo kubwa kwa viongozi Tz plus ubinafsi!!
DeleteFanyeni kazi za kuwaingizia mkate wenu wa kila siku acheni kuahangaika na siasa za Tanzania na Africa kwa ujumla. Tumeshao Afrika nzima siasa za vyama vingi ilikuwa bado, ndiyo maana kila kona watu wameuana, wamefungana,na kadha wa khadha. sisi Africa tutawaliwe Ki-sultani kama kwa Mswati au Chama kimoja maana kila mtu anakimbilia IKULU tu, wote mtaingia huko?. Vilio vya nani angie ikulu kila kona? ahaaa!!!! wanatuchanganya.
ReplyDeleteThe mdudu, mbona sisi wakuona mbali tulishayajua haya mapema hivi tujiulize kweli binaadamu kwenye kuoga kuna ukomo jibu no lazima binaadamu yoyote yule mpenda usafi kuoga sio ombi bali lazima lakini hawa wame muogesha siku mbili tu tena kwa shangwe kubwa walipotaka kumuogesha tena mwezao kakataa katakata hapo ndipo kasheshe limefumuka nguzo muhimu hiyo imetoka ya kwanza na bado nguzo ya pili yaja wakati wowote swali je nyumba itasimama bila ya NGUZO? yangu macho si Ukawa wala CCM mimi ACT Wazalendo mwendo wa Nyerere chukua pesa za mapapa + za mafisadi sambaza kwa wanyonge.......mungu mkubwa huwezi kushinda na na mungu na bado mwendo mchibuyu
ReplyDeleteKwa mtazamo wa haraka watanzania tumekuwa wagumu kupambanua mambo .tuingie kwa kina tutaelewa Prf Lipumba Dr Slaa hawa watu wana mawazo ya mbele Sana ambayo binadamu wa kawaida hawezi elewa .hv nyie inwaingia akilini mtu waliemuita mchafu Leo hii wanamkaribisha Na kumpa madaraka makubwa Ina maana ukawa asingepatikana lowasa wasingemsimamisha mgombea?
ReplyDeleteNI HERI LAWAMA KULIKO FEDHEHA. yaaani kwa nini uyalambe MATAPISHI YAKO MWENYEWE? huyu MZEE LOWASSA Hana AGENDA YA WATANZANIA Bali YAKE BINAFSI na Prof Lipumba KALIONA HIYO MAPEMA. MTU HUWEZI KUUNUNUA URAISI KWA BEI KUBWA KIASI HICHO. Utazidudishaje??? NA IKULU HAKUNA BIASHARA? JAMANI MBONA TUNAWEKA RASLIMALI YETU REHANI? lowassa ni wa kukimbiwa kama MLOZI. prof Lipumba ni uwamuzi wa KIJASIRI.
ReplyDeleteHii ni kumalizana kisiasa, kupiganaa ngwala kisiasa, na kutojali michango ya wengine, ama kweli vyama vina wenyewe.
ReplyDeleteMovie ndo kwanza inaanza.Script imeshaandikwa kilichobaki ni maigizo tu.Kweli CCM imejipanga.Kidumu Chama Cha Mapinduzi.Idumu amani na maendeleo ya nchi.
ReplyDelete