DSC_0734
Profesa Fortunata Makene wa idara ya tafiti za mikakati na machapisho wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), akifungua warsha hiyo ya siku moja iliyowakutanisha wataalamu kujadili matokeo ya utafiti wa ufanisi wa mfumo wa ugatuaji madaraka ambapo mamlaka yanapelekwa kwa wananchi (Efficiency and Effectiveness of Decentralization and Local Government Capital Development Grant LGCDC systems in Tanzania).(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Na Mwandishi wetu,
HATUA za haraka zinapaswa kuchukuliwa ili kuwezesha mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN) kutovuruga matunda ya sera ya ugatuaji madaraka uliofanywa mwaka 1998 na kuanzwa kutekelezwa mwaka 2004.

Sera ya ugatuaji madaraka imelenga kuwezesha wananchi kupanga mipango yao ya maendeleo kwa kuzingatia mahitaji yao na kupigwa jeki na serikali kuu.

Lengo la sera hiyo ni kupeleka sauti ya maendeleo kwa wananchi wenyewe badala ya sera za awali ambapo utekelezaji wa mipango ya maendeleo ulifanywa na serikali kuu.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa juma katika mkusanyiko wa wataalamu kujadili matokeo ya utafiti wa ufanisi wa mfumo wa ugatuaji madaraka ambapo mamlaka yanapelekwa kwa wananchi (Efficiency and Effectiveness of Decentralization and Local Government Capital Development Grant LGCDC systems in Tanzania) ulioendeshwa na timu ya watafiti wakiongozwa na Profesa Godius Kahyarara wa Sayansi Jamii idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Katika utafiti huo ilibainishwa kwamba pamoja na ubora wa mfumo huo uliotoa mabadiliko ya watu kujitengenezea wenyewe mipango yao ya maendeleo, sasa hivi unakabiliwa na changamoto ya BRN.

Akiwasilisha utafiti huo, mmoja wa watafiti hao, Victor Geofrey, alisema kwa kutumia methodolojia ya maswali na majadiliano walibainisha kwamba katika utekelezaji wa BRN maeneo ambapo mipango ya wananchi ilikuwa sawia na vipaumbele vya BRN miradi ilifanikiwa lakini kwingine haikuwa hivyo.
DSC_0808  
Alisema katika uwasilishaji wake wa utafiti huo uliofanyika katika mikoa mitano kwa wilaya mbili katika kila mkoa, hatari ya watanzania kurejea katika mfumo wa mwanzo wa maagizo ya juu kutekelezwa, unanukia kama kusipooitafutwa njia ya kuoanisha BRN na mfumo wa utekelezaji wenye matokeo bora ya ufanisi ya serikali za mitaa na mikoa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...