Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama hicho,Lumumba jijini Dar,kuhusiana na madai ya kauli inayodaiwa kutolewa na Mgombea wa Urais wa Chama hicho Dkt John Magufuli kuwa kupitia Ilani yake ya chama atatoa kompyuta kwa Walimu nchi nzima iwapo CCM itapita madarakani,habari ambazo Nape amezikunusha vikali na kusema hayo ni maneno ya uzusihi na kuwa Dkt Magufuli hajawahi kutamka maneno hayo popote pale.
 Nape Nnauye akionesha kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambayo imepitishwa jana Agosti 13,2015 katika Mkutano wa Chama hicho uliofanyika jana mjini Dodoma na inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 23,mwaka huu katika uzinduzi wa Kampeni.Nape amefafanua kuwa kauli yoyote iliyotoka kwa chama hicho ikidaiwa imetoka katika Ilani  ya chama cha CCM,siyo ya kweli,kwani Ilani hiyo itazinduliwa wakati wa uzinduzi wa kampeni Agosti 23" alisema na Nape kwa msisitizo.
  Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo wa CCM mapema leo jijini Dar.Picha na Michuzi Jr.


NA BAKARI ISSA WA GLOBU YA JAMII.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekanusha uvumi ulioenea sehemu mbalimbali kuwa Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chama hicho,Dkt.John Pombe Magufuli amewaahidi Walimu kuwapa Kompyuta kama CCM itapita madarakani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama hicho,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye amesema kauli hiyo siyo ya kweli na haikutolewa na Mgombea huyo wa Urais,Dkt.Magufuli.

Hatahivyo,Nape amesema kauli hiyo imetolewa kwa nia mbaya kuonyesha Chama cha Mapinduzi kimeanza ziara ya kampeni mapema.

Amesema watu walioinukuu kauli hiyo wamesema imetoka katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho,Nape amesema " Ilani ya Uchaguzi ya CCM imetoka jana Agosti 13,2015 katika Mkutano wa Chama uliofanyika jana mjini Dodoma na inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 23,mwaka huu katika uzinduzi wa Kampeni,hivyo kauli yoyote iliyotoka kwa chama hicho ikidaiwa imetoka katika Ilani yetu ya Uchaguzi,hiyo siyo ya kweli,kwani Ilani hiyo itazinduliwa wakati wa uzinduzi wa kampeni Agosti 23" alisema na Nape kwa msisitizo.

Kuhusu msimamo wa Chama cha Mapinduzi kwa wanachama wanaohama chama hicho,Nape amesema wanachama hao wanahama kwa mapenzi yao binafsi wengine wamehama kwa sababu ya kushindwa katika kura za maoni za chama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. ankal michu unahamia lini ukawa ankal??

    mdau
    UK

    ReplyDelete
  2. Kuna sababu yoyote kukana uvumi mwema kama huu?? kugawa kompyuta si jambo baya ati!!

    ReplyDelete
  3. Oil chafu inaendesha gari na abiria wanalikubali. Nape usikute ulijisahau ukatupatia oil safi na wewe ukabaki na oil chafu...tafakari.........Tanzania bila CCM inawezekana ifikapo oktoba 25

    ReplyDelete
  4. Mbona habari za Lowassa kufunika mbeya kwako wewe si habari?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...