Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi
CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji wa Mbalizi mkoa mpya wa Songwe,katika mkutano wake wa kampeni uliohudhuriwa
maelfu ya wananchi, Dr. John Pombe Magufuli amewaomba wananchi wa
Mbalizi kummpa kura za ndiyo ili aweze kuongoza watanzania na kutatua
matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii ya watanzania wa hali ya chini.
Amesema
ametumikia nchi hii kwa miaka 20 serikalini akiwa Waziri na amekuwa
mkweli na muwazi ndiyo maana ameweza kuisimamia vizuri kila wizara au
jukumu alilopewa na wakubwa wake akiwatumikia Watanzania na sasa anaomba
nafasi ya urais ili aweze kutekeleza vyema jukumu lake la kuwatumikia
Watanzania .
Aliongeza
kuwa ndiyo maana katika mchakato mzima wa kugombea urais ndani ya Chama
cha Mapinduzi alifanya kimya kimya na hakutumia fedha yoyote hivyo
hakuna mtanzania yeyote anayemdai fedha ila anadaiwa utumishi uliotukuka
wenye uaminifu, kujituma na kutetea maslahi ya watanzania na taifa kwa
ujumla katika taifa la Tanzania, Ameongeza kwamba ukitumia fedha
kuingia madarakani na kununua madaraka ipo siku utawauza uliowanunua.
Wananchi
waliokusanyika kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli
kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika stendi ya mabasi mjini
Mbalizi wakishangilia huku wakipiga makelele kwamba anatosha na anafaa
kuwa Rais na wameahidi kumpigia kura ya ndiyo.
Wafuasi
wa chama cha CCM na wananchi wakiwa wamekusanyika katika stendi ya
mabasi mjini Mbalizi wakimsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe
Magufuli,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ambapo aliwahutubia na
kuwaomba wampe kura ya ndiyo ili aweze kuwoangoza katika awamu ya tano.
Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufulia akisisitiza jambo wakati
akiwahutubia wakazi wa Mbalizi na kuendelea kusisitiza kuwa elimu
itakuwa bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne,kuongeza
maslahi ya walimu pamoja na jeshi la polisi.
Wakazi
wa mbalizi wakimsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
alipokuwa akimwaga sera za kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika
kipindi cha awamu ya tano,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye
kituo cha mabasi Mbalizi.
Maelfu
ya watu wakiwa na kiu kubwa ya kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa chama cha CCM mjini Mbalizi.
Wananchi
wa mji wa Chunya mjini wakishangilia ujio wa Mgombea Urais wa CCM Dkt
John Pombe Magufuli katika viwanja vya Saba Saba Chunya mjini kwenye
mkutano wa kampeni,ambapo Magufuli aliwahutubia wananchi hao na kuwaomba
kura ya ridhaa ya kuwaongoza kwa kipindi kijacho cha awamu ya tano.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John
Pombe Magufuli,alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Makongorosi
kuwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni.
Wananchi
wa Makongorosi wakimsikiliza kwa makini Mgombea wa Urais kupitia CCM
Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mjini hapo kwenye mkutano
wa kampeni
Wananchi
wa Makongorosi wakimshangilia Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John
Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mjini hapo kwenye mkutano wa
kampeni.
Endelea kuleta hoja za nguvu na sera za kutukwamua wananchi tunakusikiliza.
ReplyDeleteTunakutakia ushindi uchaguzi huu.
ReplyDeleteNimeipenda hiyo quote, way to go JPM
ReplyDeleteCCM na akina mama juu, oyee!
ReplyDeleteWenye kuwatafuta akina mama, ziii!