MUIMBAJI
mahiri wa muziki wa Injili anayetamba katika muziki huo, Upendo Nkone
amekubali kushiriki katika Tamasha la Kuombea amani katika uchaguzi Mkuu
unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex
Msama Nkone ni muimbaji wa kwanza wa Tanzania kukubali kushiriki katika
tamasha la hilo la Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4.
Msama
alisema wanaendelea na mchakato wa kuzungumza na waimbaji wengine ili
kuwa na idadi kubwa ya waimbaji wa Tanzania sambamba na wengine kutoka
nje.
Msama
alisema wanajipanga kualika waimbaji kutoka nchi tano za Afrika kwa
lengo la kunogesha uzinduzi huo ili ujumbe wa neno la Mungu ufike kwa
dhati.Aidha Msama alisema sambamba na waimbaji kutoka nje ya Tanzania
pia wanajipanga kutangaza amani katika mikoa 10 ya Tanzania bara.
“Tunaendelea
na mikakati ya kufanikisha Tamasha hilo ambalo litakuwa ni la aina
yake, hivyo wadau mbalimbali wasubiri tamasha hilo,” alisema Msama.
Msama
alisema Tamasha hilo litahudhuriwa na wadau mbalimbali kwa kushirikisha
wanasiasa, viongozi wa dini mbalimbali na makundi mengine kama wasanii
na wanamichezo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...