Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Selemani Ponda (katikati)akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa taarifa ya mapato ya benki hiyo katika kipindi cha robo mwaka kilichoisha mwezi Juni mwaka huu. Wengine ni Naibu Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw. Issa Hamisi (wa kwanza kushoto) na Meneja Mwanadamizi wa utafiti na uchambuzi wa biashara wa benki hiyo Bw. Joseph Mrawa (wa kwanza kulia)
Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Selemani Ponda (wa kwanza kulia)akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa taarifa ya mapato ya benki hiyo katika kipindi cha robo mwaka kilichoisha mwezi Juni mwaka huu. Wengine ni Naibu Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw. Issa Hamisi (katikati) na Mkaguzi Mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo Bw. George Binde
Benki
ya Exim Tanzania imefanikiwa kujipatia faida ya sh. bilioni 12.79
(kabla ya kodi) katika kipindi cha robo mwaka kilichoisha mwezi Juni
mwaka huu, takwimu zinazoonyesha ongezeko la faida kwa asilimia 69
katika benki hiyo.
“Ongezeko
hilo ni kubwa ikilinganishwa na faida yash.bilioni 7.56 tuliyoiopata
katika robo mwaka iliyotangulia na hivyo basi tunajisikia fahari
kutangaza faida hii mbele yenu,’’ alibainisha Afisa Fedha Mkuu wa benki
hiyo Bw. Selemani Ponda alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana.
Kwa
mujibu wa Bw Ponda faida hiyo pia ni sawa ongezeko la asilimia 28
ikilinganishwa na faida ya kiasi cha sh. bilioni 13.96 katika kipindi
cha miezi sita kwa mwaka uliopita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...