Asha Kigundula

BENDI ya muziki wa Dansi, FM Academia ‘Wazee wa Ngasuma’ Ijumaa hii ya Agosti 21 watafanya sherehe ya kuazimisha miaka 18 tangu kuanzishwa kwake itakayofanyika kwenye Ukumbi wa The Arcade House, uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana Rais wa bendi hiyo, Nyoshi El Sadaat, alisema kuwa maandalizi ya sherehe hizo yanaendelea vizuri.

Alisema kuwa siku hiyo itakuwa maalum kwa wapenzi wao kuanzia wa miaka hiyo mpaka sasa maana wataburudisha kwa kuimba nyimbo mbalimbali ambapo wataanzia saa 4 mpaka saa 9,usiku.

Alisema katika onesho hilo ambapo kampuni ya Mabibo Bear kupitia kinywaji cha Windhoek, wameandaa burudani ya kutosha kwa kupiga nyimbo za albamu zao 10 ambazo wamezitoa na kutamba.

Saadat alisema kuwa usiku huo maalum wamewaalika wanamuziki wao mbalimbali ambao waliwahi kufanya kazi katika bendi yao na kutoa hata nyimbo.

"Ni siku muhimu kwetu tokea mwaka 1997 hivyo wale wanamuziki wote ambao walikuwepo Academia watakuwepo watapanda jukwaani na kupiga nyimbo zetu zote zilizotamba.

Saadat alisema wapenzi wao watakaoingia mapema wukumbi watapata zawadi maalum ambazo wameandaa pamoja na wadhamini wao Windhoek.

Alisema kuwa hata hivyo katika usiku huo watatambulisha nyimbo zao mbili ambazo ni Dada wewe pamoja na Moyo wangu. “Niwatake wapenzi wa FM Academia kuhudhuria bila kukosa ndani ya Arcade House, Mikocheni maana siku hiyo itakuwa moto, tutatambulisha vibao viwili ambavyo ni Dada Huyo na Moyo Wangu.

Pia watakuwepo wakali waliowahi kupita kwenye bendi yetu akiwemo Ndanda Kosovo, Jose Mara, Mkabeza na wengine kibao,” alisema Nyoshi.

FM Academia ilianzishwa mwaka 1997 baada ya mmiliki wa mwanzo kabisa wa bendi hiyo, Felician Mutta kufanya makubaliano ya kuanzisha bendi na Nyoshi El Sadaat ‘Sauti ya Simba’ ambapo staa huyo alishirikiana na watu wake waliokuwa wanaishi Kenya kwa kipindi hicho.

FM Academia aliyekuwepo wakati FM Musica International ikizaliwa mwaka 1997 ndani ya Kilimanjaro Hotel jijini Dar es Salaam. Kwa sasa bendi hiyo inaundwa na vichwa hatari wakiwemo King Blaise, Pablo Masai, Ben Byevanga, Jesus, Patcho Mwamba na wengine wengi.

FM Academia iliyoanzishwa mwaka 1997 kwa jina la FM Musica International, itatumia onyesho kutambulisha nyimbo zao mbili mpya ukiwemo “Dada Wewe” utunzi wake King Blaise.

Albamu 10 ambazo toka ianzishwe bendi hiyo ni Atomic, Internet, Prisons, Fredom, Mpambe nuski, Dotnata, Dunia Kigeugeu, Heshima kwa wanawake Vuta nikuvute na Chuki ya nini.

Katika usiku huo kiingilio kitakuwa shilingi 10,000 kwa kawaida na VIP itakuwa shilingi 20,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mtupie Youtube sherehe hiyo ya miaka 18 ya FM Academia maana pia mna washabiki wengi tu ambao wanaishi ktk Diaspora na tukija nyumbani lazima tufike kusapoti wazee wa Ngwasuma.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...