Mwaka huu tumeshuhudia uhamaji wa wanachama  na viongozi  wa vyama kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine kuliko kipindi chochote katika historia ya vyama vingi  nchini Tanzania. Wengi wametafsiri hali hiyo kuwa ni ukuwaji wa demokrasia. Jambo ambalo lina ukweli wa aina fulani. 
Lakini ukiangalia kwa undani wahamaji wa pande zote wamekuwa wakitoa sababu zinazofanana, na yumkini kuhama baada ya matukio yanayofanana kutokea katika  vyama vyao. Wengi wamehama mara baada kukosa nafasi ya kupeperusha  bendera za vyama vyao  katika  uchaguzi wa  urais, ubunge au udiwani. Mara wanapokosa nafasi wanahama  vyama vyao  wakidai demokrasia imebanwa au imebakwa. 
Nimekuwa nikijiuliza , Je? Wangefanikiwa kupata nafasi ya kupeperusha bendera za vyama vyao katika nafasi walizoomba hizo sababu zingekuwepo? Maana najua wengine wamekuwa viongozi wakuu kwenye vyama  vyao na wameshiriki katika utaratibu huo huo wa kuteuana na kuchaguana katika nafasi mbalimbali na hata kushiriki kukata majina ya watu wengine, lakini kipindi hicho chote demokrasia haikubakwa. Hapa inaonyesha walivyokuwa wamekaa kwenye vyama kimaslahi zaidi na maslahi yao au matakwa yao  yasipofanikiwa wanatoa sababu mbalimbali  za kuhama, na wanapohamia kwenye vyama vingine wanataka wapewe nafasi za kugombea uongozi moja kwa moja. Watanzania tujiulize kweli hawa watu wana nia nzuri na watanzania au wanataka tu kukidhi  maslahi yao.
Nilishawahi kuguswa na mbunge mmoja aliyehama  chama  tawala akiwa mbunge karibu na bunge kumaliza muda wake. Watu walimshangaa, na baadhi ya wenzake wakamwambia  mbona unahama kipindi hiki na kuacha kiinua mgongo cha ubunge.  
Yeye alisimamia msimamo wake na  alichokuwa anakiamini na sio maslahi. Aligombea  ubunge kwa chama cha upinzani  katika jimbo  moja la Dar es Salaam  kula zake hazikutosha na nasikia mwaka  huu anagombea ubunge nyumbani kwao. Huyu hakusubiri mpaka  jina lake likatwe ndio ahame. Alifanya alichokiamini  sio maslahi kama wengine wanavyofanya sasa. Kuna watu wamehama  vyama vitatu kwa wiki moja wakitafuta nafasi ya ubunge. Kuna watu wamehama vyama  kwa makubaliano tu wapewe nafasi ya kugombea uongozi. Mimi najiuliza watu hawa kweli wana nia ya dhati ya kuwatumikia watanzania au ni wanachama maslahi?

Utagundua wanachama maslahi katika vitu vingi, kwanza wanakuwa wanatanguliza agenda zao na si za chama, pili hawathubutu kuvaa mavazi rasmi ya  vyama vyao. hawataki kupambanuliwa kuwa wanachama wa chama walichojiunga nacho kupitia  vyazi rasmi la chama hicho. 
Wote tunajua CCM wanavaa mashati ya kijani, na Chadema wanavaa kombati kama  vyazi rasmi la vyama vyao. Lakini leo hii ukiona mtu anadai kuwa yeye ni mwanachama wa Chadema au CCM au NCCR au TLP au NLD na amepewa dhamana ya kupeperusha  bendera ya   chama lakini anaogopa kuvaa  vazi rasmi   la chama husika(hata kofia tu), ujue hapo kuna tatizo. Watanzania  tuangalie kwa makini, wanachama tuangalie kwa makini tusije tukakuta  tumealika mamluki katika vyao vyetu. Kazi kwetu kutafakari na kufanya uamuzi sahihi tarehe 25/10/2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Well said UKAWA wote ni mamruki kura yangu piga uwa inaenda kwa MAGUFULI coz hatakama anatoka CCM mimi naamini yeye ndio ataleta mapinduzi ya kweli ndani ya CCM na serikali yake kwa ujumra maana huyu mtu hana masihara na mtu wala fisadiz na kwa upande mwingine CCM imejifunza kutokana na makosa waliojitakia wenyewe kwa kuwapa uhuru mkubwa MAFISADI wachache ambao ni hatari kwa taifa letu........kwa mtazamo wangu wa hali ya juu kabisa pasipo kumung'uunya maneno kama MAGUFULI akishinda na kuapishwa kuwa RAIS WA WATANZANIA basi wale wote MAPAPA FISADIZ wajiandae kufilisiwa na kwenda UKONGA NA KEKO na hii ndio itakua team ya MAGUFULI (wmkuu) Mwakiyembe (wwshule) Makamba (wwumeme) Muhongo (ww mahakama ya mafisadi Makongoro patamu hapo) wapesa Mwigilu na wa sheria Sita na wa mwisho kwa upande wangu ni Kunjombe wa mambo ya ndani na ikumbukwe huyu hatokua na team kubwa zaidi ya 20au25 haya kazi kwenu wadau ongezeeni hiyo team ili iwe kiwembe zaidi.

    ReplyDelete
  2. Kufuatana na katiba yetu na taratibu tulizojiwekea wanasiasa hutafuta ridhaa ya kuongoza kutoka kwa wananchi kila baada ya miaka mitano. Sasa hivi kwa sababu ya vyama vingi unapofungiwa fursa ya kugombea nafasi katika kura ya maoni njia inaweza kufunguka katika chama kingine, kwa maana ya kuwa unaweza kujaribu bahati kwenye chama kingine. Hii ruka ruka si rahisi nyakati hizi kwa sababu wapiga kura na wagombea wameamka wanataka kuona haki zaidi katika uteuzi, vyama vya kuunguna kama ukawa vimeshagawana nafasi zilizopo. Kutumia ushawishi wa kisiasa kujihakikishia nafasi kutaisha hata mambo ya kupita bila kupingwa kunaenda kunapungua mwisho kutaisha kabisa. Mchuano umekuwa mkali wagombea wapya wapo siasa zinabadilika.

    ReplyDelete
  3. Mwalimu Nyerere alishawahi kuvaa kijani? Hoja yako bado ina mapungufu!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...