Hali ya ugonjwa wa kipindupindu mkoani Morogoro imeendelea kuwa tete baada ya idadi ya wagonjwa wa kipindupindu kungezeka hadi  kufikia wagonjwa 45 ambao wanaendelea na matibabu katika kambi maalum katika hospitali ya sabasaba mjini Morogoro.

 
Akizungumza na mtandao huu afisa afya mkoa wa Morogoro Carlesilas Lyimo amesema kutokana na kasi ya ongezeko la kipindupindu maafisa afya wamefanya operesheni katika maeneo mbalimbali yanayotoa huduma za chakula na vinywaji na kufanikiwa kukamata na kumwaga pombe za kienyeji zaidi ya lita 770, kuwachukulia hatua wafanyabiashara wa chakula wanauza vyakula bila utaratibu pamoja na kutoa dawa za kuwakinga na kipindupindu majumbani kwa watu 410 wengi wao wakitokea kata ya kilakala.
 

Nao wananchi wa mji wa Morogoro wameeleza wasiwasi wao juu ya kuongezeka idadi ya wagonjwa wa kipindupindu ambapo wametupia mamlaka ya maji safi na maji taka Moruwasa kushindwa kutoa huduma ya maji kwa wananchi katika baadhi ya maeneo hali inayosababisha wananchi kulazimika kutumia maji ya mito ambayo si salama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...