Chalila Kibuda,Globu ya jamii
UGONJWA wa kipindupindu unazidi kusambaa katika manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi habari leo Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni,Aziz Msuya watu waliofariki katika manispaa hiyo watatu.
Amesema idadi ya wagonjwa katika manispaa imezidi kuongezeka kutoka 34 hadi kufikia 43.

Amesema dalili za huo ni  homa kali ,kuharisha pamoja na kutapika na kuongeza kuwa mtu akifikia dalili hizo awahi katika kituo cha afya.

Aidha amesema kujiepusha na ugonjwa huo ni kuzingatia usafi wa vyakula ,maji pamoja na kunawa mikono kwa usafi wakati wa kula.

Msuya amesema watu waliokuwa wamelalazwa na ugonjwa huo watatu wamerusiwa.

Katika zahanati ya Mburahati wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa ni  21.

Muuguzi Mkuu wa Zahanati hiyo, Nusra Kessy amesema kuwa wagonjwa hao wanaendelea kutibiwa katika zahanati hiyo.
  Usafi ukiendelea katika Zahanati ya Mburahati katika kukabiliana na Ugonjwa Kipindupindu mara baada ya Globu ya Jamii kutembelea kujionea hali halisi ya ugonjwa huo leo jijini Dar es Salaam.
 Wakati ugonjwa wa kipindupindu ukiwa umeshika kasi lakini watu bado wanakula holela kama walivyokutwa na Kamera yetu leo jijini Dar es Salaam.
Usafi wa Mazingira katika Zahanati ya Mburahati ukiendelea kama walivyokuwa na Globu ya Jamii leo jijini Dar es Salaam.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...