
Mgombea
urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisaini fomu za
hati ya Kiapo kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jijini Dar
es salaam leo Agosti 19, 2015. Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya
urais anatakiwa kusaini katika mahakama kuu jijini Dar es Salaam .

Mgombea
mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni
akisaini fomu za hati ya Kiapo kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya
Tanzania, Jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2015. Kushoto kwake ni
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama
hicho, Mh. Edward Lowassa.

Mgombea
urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mweza
wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwa kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya
Tanzania, Jaji Suleiman Said Komu (mbele) wakati wa kusaini fomu za hati
ya Kiapo, leo Agosti 19, 2015. Kulia ni Mwanasheria wa CHADEMA, Mh.
Mabere Marando.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...