Na Demetrius Njimbwi – jeshi la Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu, amewataka Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa na Wilaya, kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili kuzitatua changamoto zinazojitokeza katika jamii yetu hatua ambayo itasaidia kuutokomeza uhalifu na wahalifu.
Kauli hiyo ameitoa mjini Dodoma, jana wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wilaya, mafunzo ambayo yatawajengea uwezo wa kiutendaji katika kukabiliana na uhalifu na wahalifu.
Hata hivyo, IGP Mangu, amesema kuwa, ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ni wazi kuwa, kasi ya utendaji kazi iongezeke ili kujenga taswira bora ya kiutendaji ya Jeshi la Polisi na kwamba suala la utoaji wa huduma bora kwa mteja ni la lazima hususan katika Nyanja ya upelelezi, alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI) Diwani Athumani, amesema kuwa, mafunzo haya ya siku mbili yatasaidia kuongeza kasi ya utendaji na kwamba Kamisheni ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini imeandaa mafunzo haya ili kuongeza tija katika masuala ya upelezi.
Ameongeza kuwa, jumla ya Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wilaya 205 wanashiriki katika mafunzo haya na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi hatua ambayo kwa pamoja itasaidia kuzuia makosa ya uhalifu na wahalifu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu, akizungumza na Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wilaya (hawapo pichani) wakatia akifungua mafunzo ya siku mbili yanayofanyika mjini Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu, akizungumza na Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wilaya, wakatia akifungua mafunzo ya siku mbili yenyelengo la kuwajengea uwezo wa kiutendaji yanayofanyika mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI) Diwani Athumani, akitoa neno kwa Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wilaya (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo ya siku mbili inayofanyika mjini Dodoma. (Picha na Demetrius Njimbwi - Jeshi la Polisi).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...