Timu ya Moro Kids imeukwaa uchampioni wa mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Morogoro baada ya kuwafunga Kihonda 2-1 katika mchezo wa funga dimba uliopigwa jana kwenye uwanja wa Shujaa mjini Morogoro.

Ushindi huo kwenye mchezo wa jana uliohudhuriwa na mashabiki wengi uliwawezesha Moro Kids kufikisha pointi sita wakifuatiwa na timu ya Tecfort iliyohitimisha mashindano hayo ya mkoa ikiwa na pointi tatu.

Wakati huo huo chama cha soka mkoani Morogoro (MOREFA) kimetangaza kikosi cha wachezaji 20 kitakacho uwakilisha mkoa huo katika mashindano ya taifa yaliyopangwa kuanza kutimua vumbia kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Septamba 11 hadi 21.

Katibu Mkuu wa MOREFA Emmanuel Kimbawala amesema kikosi hicho kilichochaguliuwa wakati wa michuano hiyo mkoani Morogoro kimeundwa na wachezaji wenye vipaji na ku0nyedha dhamira ya dhati ya kuweza kutwaa tena ubingwa wa Airtel Rising Stars ngazi ya taifa mwaka huu.

Lengo la mashindano ya Airtel Rising Stars ni kuwapa fursa wachezaji chipukizi wa soka, wasichana na wavulana, kuonyesha vipaji vyao na hatimaye kuweza kuonekana na kuchaguliwa kuchezea timu mbalimbali. matunda ya Airtel Rising Stars yanaonekana katika timu za taifa za vijana na Twiga Stars.

Mwaka huu mashindano ya Airtel Rising Stars yanajumuisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke, Ilala Mbeya na Mwanza kwa timu za wasichana na wavulana huku mkoa wa Morogoro ukishirikisha wavulana peke yake wakati Arusha ni wasichana tu.
Naodha wa timu ya Moro Kids Dissy Job akinyanyua kombe la ubingwa la Airtel Rising Stars baada ya kutawazwa mabingwa wa mkoa wa Morogoro.
Timu ya Moro Kids waki pozi na kombe la ubingwa baada ya kutawazwa mabingwa wa mkoa wa Morogoro katika mashindano ya Airtel Rising Stars.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...