Na Mwashungi Tahir
-Maelezo Zanzibar
Mwanahabari Abdallah Abdulrahman Mfaume amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) kwenye mkutano mkuu wa jumuiya hiyo uliombatana na Uchaguzi wa viongozi wapya katika ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
Bw. Mfaume aliibuka mshindi baada ya kupata kura 40 na kumshinda mpinzani wake wa karibu Bw. Suleiman Abdalla ambae alipata kura tisa.
Katibu Mtendaji wa ZPC Faki Mjaka ambaye hakuwa na Mpinzani alipata kura 46 na Naibu Katibu Mwinyimvua Nzukwi alipata kura 37 baada ya kumshinda Takdir Ali aliyeata kura 13.
Makamo Mwenyekiti wa Jumiya hiyo ni Abdalla Pandu aliyepata kura 28 na kumshinda Rahma Suleiman aliyepata kura 23. Mshika fedha Halima Tamim Thuwein aliyekuwa Mgombea pekee alipata kura 49.
Wajumbe sita wa kamati tendaji ni Aziza Hassan, Ghania Mohammed, Mwashamba Haji Juma, Ishaka Omar, Maulid Hassan Kipevu na Saleh Hassan.
Wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu huo, wito ulitolewa kwa waandishi wa habari nchini kulinda maadili ya kazi zao ikiwemo kutumia kalamu zao vizuri hasa katika kipindi hiki wanapoelekea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Imeelezwa kuwa ikiwa waandishi watatumia vibaya kalamu zao basi wanaweza kuvuruga hali ya amani na utulivu na kuweka nchi katika hali ya machafuko.
Hayo yalielezwa na Meneja Bima ya Maisha Tawi la Zanzibar Aisha Rubenic Makorogo, wakati akifungua mkutano huo.
Alisema, kazi muhimu ya wanahabari ni kuona wanaendelea kutoa elimu kwa jamii na kutokubali kutumiwa vibaya na watu wenye maslahi binafsina badala yake wafanye majukumu yao kwa kutenda haki kwa pande zote ili nchi iweze kuvuka salama.
Aidha alisema, tasnia ya habari ni tasnia muhimu katika jamii ambayo inategemewa na kila mtu kwani inaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa wanachi wanaoishi mijini na vijijini kupata habari zinazotokea nchini kupitia vyombo wanavyofanyia kazi.
Katibu Mkuu msaafu wa Jumuiya ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) Suzan Peter Kundambi katikati akitoa taarifa ya mwaka kwa Wanachama wa Jumuiya hiyo katika mkutano wa Mwaka wa ZPC ulioambatana na uchaguzi. Mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
Wajumbe walioshiriki uchaguzi wa Jumuiya ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) wakipiga kura kuchagua uongozi mpya katika mkutano wa Mwaka wa Jumuiya hiyo ambao uliambatana na uchaguzi huo ambao uliofanyika ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
Kura zikihesabiwa
Katibu Mpya wa Jumuiya ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) Faki Mjaka akiomba kura kwa Wanachama (hawapo pichani)kabla ya kufanyika Uchaguzi huo. Katibu huyo anashika nafasi ya Suzan Peter mara baada ya kushika nafasi hiyo katika mkutano wa Mwaka wa Jumuiya hiyo uliambatana na uchaguzi huko ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
Mweyekiti mpya wa Jumuiya ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) kulia akipongezana na aliyekuwa mpinzani wake katika nafasi ya Uenyekiti Suleiman Abdallah mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti mpya katika uchaguzi uliofanyika ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...